Na Pamela Mollel,Arusha 

Wananchi wa kata ya Seela Sing'isi halmashauri ya Meru Mkoani  Arusha, wamempongeza Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule mpya ya Sekondari Madiira iliyogarimu Milioni 584

Wakizungumza kwa nyakati tofauti shule hapo,wananchi hao wameeleza namna ambavyo serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo ya Elimu 

Elieneza Kitomari anasema shule hiyo inamiundombinu ya kisasa ikwemo madarasa na maabara za masomo yote ya Sayansi 

Aliongeza kuwa anafurahishwa na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan namna anavyo anawakumbuka hata wananchi wa vijijini kwa kuwapelekea miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya shule ya Sekondari Madiira

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Joel Sidael anasema miundombinu ya shule hiyo imekamilika kwa asilimia 70 na wazazi wameshachukua fomu za kujiunga na kidato cha kwanza ambapo wanafunzi 100 tayari wameshajiunga na shule hiyo wakiwemo wasichana 50,wavula 50

Shule hiyo ya Sekondari imejengwa na serikali kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya Elimu Sekondari (SEQUIP)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...