Na. Peter Haule, WF, Morogoro

Wasanii wanaoshiriki zoezi la kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) lililopata semina ya elimu hiyo, wametakiwa kuwa mfano kwa jamii kwa kuzingatika sheria na kanuzi za uendeshaji wa shughuli za kutoa elimu ya huduma ndogo za fedha.

Hayo yameelezwa mkoani Morogoro na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, wakati akifunga Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii TACCI, yaliolenga kutoa elimu ya fedha kwa njia bunifu ya sanaa.

“Wizara ya Fedha tunajipanga kwenda vijijini kutoa elimu ya fedha, kwa kuwatumia wasanii wa ngoma, nyimbo na maigizo na tunatamani kuona wananchi wengi zaidi wanafikiwa kwa njia rahisi lakini yenye ufanisi’’ alisema Bi. Hiza.

Amewataka wasanii kuendelea kubuni sanaa zinazoelimisha jamii kwa kuwa kazi za sanaa zinamvuto na hazichoshi kuzisikiliza na kuzitazama hivyo zikitumiwa kwa malengo chanya zitatoa mchango mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), Mtaalamu wa Sanaa za Jukwaani, Bw. Harrison Kisaka, alisema kuwa elimu waliyoipata mwanzo ilikuwa na lengo la kuisaidia jamii hasa vijijini lakini imekuwa msaada mkubwa kwa wajumbe wote wa mafunzo hayo, hivyo akaahidi kuwa watakuwa chachu ya uelewa wa elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka.

Alisema kuwa pamoja na mambo mengine watatumia muda mrefu kuigiza, kuimba na kubuni sanaa ya ngoma zitakazo jikita kwenye elimu ya fedha ili na wao waweze kutoa mchango wao kwenye Taifa.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza na Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji Elimu ya Uraia TACCI, Bi. Aline Augustin, wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa semina kwa Wasanii kutoka Shirika hilo yaliyolenga utoaji wa elimu ya fedha vijijini, iliyofanyika mkoani Morogoro.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akifunga mafunzo kwa Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji Elimu ya Uraia (TACCI), wanaolengwa kutoa elimu ya fedha vijijini, mafunzo hayo yalifanyika mkoani Morogoro.
Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia TACCI, Bi. Aline Augustin baada ya kumalizika kwa mafunzo kwa Wasanii kutoka Shirika hilo yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mtaalamu wa Sanaa za Jukwaani kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), Bw. Harrison Kisaka, akiishukuru Wizara ya Fedha kwa kuona umuhimu wa kutumia sanaa katika kutoa elimu ya fedha kwa jamii, wakati wa kufunga mafunzo kwa wasanii wa shirika hilo mkoani Morogoro.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (katikati), Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia TACCI, Bi. Aline Augustin (kushoto) na Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na TACCI baada ya mafunzo ya elimu ya fedha kwa njia ya sanaa yaliyofanyika mkoani Morogoro.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...