Dar es Salaam. Tarehe 31 Januari 2024: Katika jitihada zake za kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali nchini, Benki ya CRDB imezindua msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ na kutenga jumla ya zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 470 mamilioni kwa wateja wake mwaka huu.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul amesema lengo la kampeni hiyo ni kujenga utamaduni wa matumizi ya kidijitali katika huduma za kifedha ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuondokana na matumizi ya fedha taslimu.
“Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaihamisha dunia kutoka kwenye miamala ya fedha taslimu kwenda ile isiyohusisha fedha taslimu yaani cashless economy. Tanzania hatupaswi kuachwa nyuma, ni lazima twende na mabadiliko hayo tena kwa kasi inayostahili,” amesema Bonaventure.
Kushiriki na kujiwekea nafasi ya ushindi katika kampeni hiyo mteja anatakiwa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kibenki ikiwamo kulipia ankara za maji, umeme au visimbusi vya television, ada, malipo ya manunuzi, kutuma pesa, kulipia kodi, mikopo ya kidijitali, kutoa fedha kwa ATM au CRDB Wakala, kulipia bima ya vyombo vya moto, na huduma nyenginezo.
Kushiriki na kujiwekea nafasi ya ushindi katika kampeni hiyo mteja anatakiwa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kibenki ikiwamo kulipia ankara za maji, umeme au visimbusi vya television, ada, malipo ya manunuzi, kutuma pesa, kulipia kodi, mikopo ya kidijitali, kutoa fedha kwa ATM au CRDB Wakala, kulipia bima ya vyombo vya moto, na huduma nyenginezo.
“Kwa kadri mteja atakavyokuwa akifanya miamala mingi zaidi ndivyo atakavyojiwekea nafasi ya ushindi,” amesema Bonaventure huku akibainisha kuwa katika kampeni hiyo itakayoenda hadi mwisho wa mwaka, kutakuwa na washindi wa gari aina ya Nissan Dualis watakaopatikana kila baada ya miezi mitatu, huku zawadi za bajaj na pikipiki zikitolewa kwa mshindi wa kwanza na wa pili kila mwezi.
Aidha, katika msimu huu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ya SimBanking’, Benki ya CRDB imetenga zawadi za kompyuta mpakato kufikia 10 kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu, zawadi za simu janja, pamoja na fedha taslimu.
Pamoja na zawadi hizi Benki hiyo pia imetenga kiasi cha Shilingi milioni 200 zitakazotolewa kupitia Tembo Points ambazo mteja atakuwa akikusanya kila anapofanya muamala. Wateja wataweza kubadili Tembo Points zao kuwa fedha na kuzitumia kulipia huduma au bidhaa.
Bonaventure amewakumbusha wateja wa Benki ya CRDB ambao hawajakamilisha usajili wa huduma za SimBanking kukamilisha mchakato huo ili wakidhi vigezo vya kujishindia moja kati ya zawadi zilizotangazwa na kuwakaribisha wananchi wengine kufungua akaunti kwa vigezo nafuu sana na kuunganishwa na SimBanking ili kufurahia huduma zilizoboreshwa zaidi.
Benki imeendelea kuiboresha huduma yake ya SimBanking ili kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa na uzoefu ulio bora zaidi kwa wateja. Mwaka jana, tulizindua SimBanking App iliyoboreshwa ambayo inatumia akili mnemba (Artificial intelligence), ianyoiwezesha kuwa na uwezo mkubwa katika utambuzi wa tabia na mahitaji ya mteja pindi anapotumia.
Mapema mwaka huu Benki ya CRDB imeongeza huduma mbili mpya ndani ya SimBanking ikiwamo huduma ya malipo kupitia Msimbomilia wa Taifa (TANQR) ikimuwezesha mteja kufanya malipo kwa watoa huduma wote wa Benki ya CRDB na hata mitandao ya simu. Huduma nyengine ni ile ya kujitengenezea Tembo Virtual Card mahsusi kufanikisha miamala ya kieletroniki popote pale duniani kwa kushirikiana na Union Pay.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...