Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza Ng' wilabuzu Ludigija amewataka wazazi wenye watoto waliofikisha umri wa kwenda shule kuwapeleka shule kusoma na kuacha kulazimisha kufuga na kulimaDC Ludigija ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Sumve iliyopo wilayani humo ndipo pamoja na mambo mengine akawataka kuhakikisha jumatatu wanawapeleka shule watoto wao

Ameongeza kuwa kuanzia jumatatu atatembelea shule za wilaya hiyo kuangalia mahudhurio ya watoto na watakaobainika kushindwa kuripoti atahakikisha wazazi wao wanachukuliwa hatua za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...