Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema Serikali itaendelea kuratibu na kusimamia shughuli za Serikali ili kuleta maendeleo nchini.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari kuhusu maendeleo na mafanikio ya Wizara hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema Serikali inaratibu na kusimamia maashimisho ya sherehe za kifaifa na kukabiliana na Maafa kwa faida ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Amesema Wizara hiyo ina jukumu la  kusimamia na kuwajengea uwezo Wananchi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inachangia kuboresha maisha na kupunguza umasikini.

Alifahamisha kuwa TASAF imehusika na ujenzi wa Miundombinu  mbalimbali ya kijamii, ikiwemo Skuli na Vituo vya afya ili kuleta maendeleo na kusogeza huduma karibu na Wananchi.

Alisema kuwa kupitia TASAF jumla ya  Shilingi Bilioni 14.3 zimetolewa kwa kaya 48,142 kwa ajili ya ruzuku za kuwawezesha kumudu mahitaji ya msingi ya kimaisha pamoja uhakika wa upatikanaji wa chakula, huduma za afya na elimu kwa watoto.

Alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu jumla ya Miradi 266 imetekelezwa na kutoa ajira za muda ambapo jumla ya Shilingi 8,106,678,139 zimetumika kwa malipo ya ujira na ununuzi wa vifaa.

Alisema Serikali inaendelea kuimarisha uwezo jamii kukabiliana na maafa kwa kutoa elimu katika makundi mbali mbali ya kijamii na kutoa tahadhari juu ya matukio ili Wananchi kuchukua hatua stahiki mapema kabla na wakati wa kutokea.

Alifahamisha kuwa katika kudumisha Muungano jumla ya hoja 25 zimeibuliwa na kujadiliwa na mpaka sasa hoja 18 zimepatiwa ufumbuzi miongoni mwa hoja hizo ni Uvuvi kwenye Ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu.

Alisema Serikali zote mbili zimeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, katika kipindi hiki zaidi ya miradi 10 ya Muungano inatekelezwa Zanzibar na imekuwa ikileta mabadiliko chanya katiaka upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...