NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MKURUGENZI
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bw. Nassor Shaaban, amesema,
Mfuko huo uko mbioni kuanzisha SKIMU ya
kulipa Fidia kwa mfanyakazi atakayeumia kazini kama ilivyo kwa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF) ambao unatoa huduma hiyo kwa upande wa Tanzania Bara.
Bw.
Shaaban ameyasema hayo wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za
Umma za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), lililofanyika pembezoni mwa Maonesho ya 10 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamanzi, Zanzibar.
Maonesho
hayo ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar, yalianza Januari 10, 2024 na yatafikia kilele Januari 19, 2024.
“Katika
utayarishaji wa kuanzisha Mafao (skimu)
haya ya mfanyakazi atakayeumia kazini, tumekuwa tukishirikiana sana na wenzetu
wa WCF ili kupata uzoefu kutoka kwao ambao, wenzetu wana uzoefu wa miaka mingi
na wanasifika kwa kutoa mafao mazuri," amefafanua Bw. Shaaban.
Amesema,
tayari wamepatiwa elimu, uzoefu, sheria na kanuni, zinazosimamia masuala ya
fidia kwa wafanyakazi, ili na wao waweze kufanya matayarisho mazuri ya
kuanzisha chombo kama WCF.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John
Mduma, amesema, Mfuko huo umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake
katika kulipa fidia kwa wafanyakazi walioumia, kuugua ama kufariki kutokana na
kazi na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na nchi za Afrika
“WCF
imekuwa Mfuko wa kuigwa barani Afrika, ukanda wa SADC na Afrika Mashariki, na
kama uzoefu huu tunausambaza katika nchi hizo, tumeona ni vema uzoefu huu pia
tuweze kuusambaza kwa ndugu zetu wa Zanzibar na ndio maana tumekua na
ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha na wao wanafikia azma yao ya kutoa fao
hilo," amefafanua Dkt. Mduma.
Aidha
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, amesema, wananchi wana
matumaini makubwa ya kuona ushirikiano wa Taasisi za Umma za Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zile za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
unaleta tija katika maisha yao.
“Maendeleo
ya nchi hii yanapitia katika mikono yenu, katika taasisi zenu, mashirikiano
haya yaonyeshe kwa uwazi kwa wannachi kama ambavyo wameanza kusema kwenye
ameneo mengi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Nane, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Hussen Ali Mwinyi, zimekuwa zinajibu
mahitaji na kiu ya Watanzania kila sehemu.” Amefafanua.
Kwa
upand wake, Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Umma za Serikali ya Jmahuri ya
Muungano wa Tanznaia, Bi. Latifa Khamis, ambaye pia ni Mkuurgenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), amesema, pamoja na mambo
mengine, kongamano hilo lina lengo la kuwawezesha wakuu wa taasisi za SMT na
SMZ kubadilishana uzoefu na kujadiliana namna ya kushirikiana baina ya taasisi
wanazoziongoza.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF),
Bw. Nassor Shaaban wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tnazania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ), kwenye viwanja vya Namanzi, Zanzibar
Dkt.
Mduma (katikati) na Bw. Shaaban (kulia) wakiwa kwenye kikao hicho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...