Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini amekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Mil. 105,000,000 kwa taasisi ya vikoba Tanzania (BUTA VIKOBA ENDELEVU), kama sehemu ya kuviwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wadogo. ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Abood amekabidhi hundi hiyo Februari 23 mwaka huu wakati akifungua mafunzo ya semina kwa wanachama wa Buta Vikoba Endelevu ambapo mafunzo hayo yalikusanya vikundi mbalimbali vya ujasiriamali kutoka ndani ya Mkoa WA Morogoro.

Aidha, Mbunge huyo amesema katika kuimarisha vikundi ndani ya Manispaa ya Morogoro wamefanikiwa kuvigikia vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 300, ambapo idadi kubwa kati ya hivyo vilianza na mitaji midogo kama Mil. 1 hadi Mil. 5 na sasa vina mitaji mikubwa ya kuanzia Mil. 20 hadi Mil. 25.


Vilevile, Abood ametumia jukwaa hilo kuwaasa vijana na kinamama wenye ujuzi wa fani mbalimbali kuchangamkia fursa za kuanzisha au kujiunga katika vikundi vya ujasirimali ili kuwezeshwa kiuchumi na taasisi za kifedha Kama Banki.


“Kwa nafasi ya upendeleo nitumie jukwaa hili kutoa rai kwa vijana wa Manispaa ya Morogoro, Mkoa na nchi nzima, kupitia semina hii kuchangamkia fursa mbalimbali za uanzishwaji au kujiunga katika mbalimbali vya ujasiriamali ili kuiwezesha Serikali na taasisi za kifedha kutoa mikopo nafuu kwa vikundi hivyo ili kurahisisha vijana kujiajiri". Amesema Abood

“Vijana na kimama ndio jeshi kubwa linalotegemewa kujenga uchumi wa nchi hii, tunachelea kusema vijana na kinamama wa kiimarika kiuchumi basi nchi imemarika na ipo salama kiuchumi. Vijana tuache kulalamika, tuunde vikundi, tuombe mikopo ili tuweze kujiajiri kuliko kukaa na kutoa lawama kwa Serikali. Na kama hatuwezi basi tuwafuate Wana Buta Vikoba Endelevu watupe ujanja na siri iliyowasaidia hadi kufika hapa”. Amesema Abood.


Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kitendo cha kuendelea kutoa fedha na maagizo mbalimbali kwa taasisi za kifedha pamoja na Halmashauri zote nchi, kutenga fedha kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vidogo vidogo vya wajasiriamali.


Naye Semeni Gamabambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Buta Vikoba Endelevu amesema pamoja changamoto si kikwazo kwao cha kupata maendeleo, kwani tangu kuanzishwa kwake taasisi hiyo hadi sasa, wana wanachama 9900 na wanamiliki mtaji wa zaidi ya 1,000,000,000




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...