Na Mwandishi wetu Dodoma

Kijana mwenye umri wa mika 35 Mhandisi Alpha Mbennah, mkazi wa Jiji la Dodoma amebuni mfumo wa kidigitali wa kuhifadhi taarifa za kitaaluma za wanafunzi kuanzia ngazi ya msingi mpaka vyuo vikuu ujulikanao kama SPIN-ED (Academic Performance Management System).

Akizindua mfumo huo leo Februari 22,2024 Jijini Dodoma mbele ya wanahabari Mha. Mbennah amesema kuwa mfumo huo unamruhusu mwalimu katika ngazi tajwa kuweza kukusanya na kuingiza alama za mwanafunzi aliyesajiliwa katika mfumo kisha huchukua alama hizo na kuzichakata kwa kutengeneza wastani uliopimwa au usiopimwa kubaini gredi ya alama hizo, yaani A, B, C, n.k.

“Pia huu mfumo unaweza kubaini wastani wa darasa husika, nafasi aliyoshika kila mwanafunzi katika somo husika na katika darasa kwa ujumla pamoja na kutengenza ripoti ya maendeleo ya kitaalamu kwa kila mwanafunzi aliyesajiliwa kwenye mfumo, katika darasa husika, kutoa maoni ama comments zinazohusiana na ufaulu wa mwanafunzi na kuchora grafu ya maendeleo ya kitaaluma kwa kila mwanafunzi,” amesema.

Amesema vyote hivyo hufanywa moja kwa moja huku akiongeza kuwa hivo ni baadhi ya vipengele viivyopo katika mfumo wa SPIN-ED.

“Niseme tu kwamba vina umuhimu mkubwa sana katika uchakataji wa taarifa za kitaaluma za wanafunzi kwani huwasaidia walimu na wadau mbalimbali wa elimu kufanya maamuzi mbalimbali na hatimae kuongeza ufanisi katika mbinu za ufundishaji na ujifunzaji,” amesema.

Amesema sababu kubwa yakufanya ugunduzi wa mfumo wa SPIN-ED kutokana na changamoto alizoziona wakati akiwa mwalimu wa kujitolea katika moja ya shule hapa nchini, hususan katika uandaaji wa ripoti za maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Mfumo huo wa SPIN-ED aliugundua mwaka 2021 na kuanza kufanya kazi mwaka huohuo ambapo mpaka sasa shule 3 zinatumia mfumo huo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...