Mtu mmoja amefariki na wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari la abiria aina ya Tata yenye namba za usajili T 596 EAF inayofanya safari zake Morogoro _Mlimba kugongana uso Kwa uso na bajaji iliyokuwa inatokea Mindu kuelekea Morogoro Mjini.

Mmoja wa Majeruhi hao amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Mindu Barabara kuu ya Morogoro _Iringa majira ya asubuhi  moja asubuhi  huku chanzo chake kikiwa ni uzembe wa dereva wa basi la abiria kuhama upande wake bila kuchukua tahadhari na kuigonga bajaji hiyo

Daktari Kutoka kitengo Cha dharula hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro Joseph Kwai amekiri kupokea mwili wa marehemu ambaye ni mwanamke aliyekuwa  abiria wa bajaji huku  majeruhi hao  wakitokea kwenye basi na bajaji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...