* Aelezea Mikakati ya Serikali katika kukuza Ustawi wa Watu wenye Ulemavu nchini

Na: Mwandishi Wetu - DODOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amefanya mazungumzo na Mtaalam wa kujitegemea wa masuala ya haki za Watu wenye Ualbino kutoka Umoja wa Mataifa (UN Independent Expert on the Enjoyment of rights by Persons with Albinism), Bi. Muluka-Anne Miti-Drummond leo Februari 6, 2024, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na Mpango Kazi wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino, Kujadili Rasimu ya Mpango Kazi wa Watu wenye Ualbino na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa Watu wenye Ualbino na ufikiwaji wa huduma ya afya, haki zao na elimu jumuishi.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Waziri Ndalichako amebainisha kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Watu wenye Ualbino (TAS)pamoja na Wadau wa maendeleo wanaoshughulika na masuala ya Watu wenye Ualbino nchini wameandaa rasimu ya Mpango Kazi wa Taifa kwa Watu wenye Ualbino (MTAWWU, 2023/2024 – 2027/2028) ambao umejikita katika kutokomeza ubaguzi na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino.

Vile vile, Prof. Ndalichako amesema Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha usawa, haki, fursa, huduma bora na ustawi kwa watu wenye ulemavu ikiwamo huduma ya afya, haki ya elimu, ajira, miundombinu rafiki na upatikanaji wa vifaa saidizi.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichakoakiwa kwenye mazungumzo na Mtaalam wa kujitegemea wa masuala ya haki za Watu wenye Ualbino kutoka Umoja wa Mataifa (UN Independent Expert on the Enjoyment of rights by Persons with Albinism), Bi. Muluka-Anne Miti-Drummond (kushoto) walipokutana kwa lengo la kujadili kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino, jijini Dodoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...