Na BALTAZAR MASHAKA, MAGU


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeibomoa CHADEMA wilayani Magu baada ya aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kata ya Magu mjini, Titus Gabriel kujiunga na CCM.


Gabriel akiongozana na Said Kishiwa pia mwanachama wa CHADEMA wametangaza uamuzi huo wa kujiunga na CCM leo katika maadhimisho ya miaka 47 yaliyofanyika kimkoa wilayani Magu.
Akizungumza na Uhuru Gabriel amesema wamejiengua CHADEMA na kujiunga na CCM kwa sababu ya ubinafsi wa viongozi wa juu wa chama hicho lakini pia kazi nzuri zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

"Chama nilichokuwa nikikipigania hakikutaka kushuka chini na kujishusha kwa wananchi kufanya kazi na ubinafsi wa viongozi wa CHADEMA umesababisha nijiunge na CCM bila kushawishiwa na mtu" amesema.

Gabriel amesema kiongozi lea sababu zilizomvuta kujiunga na CCM ni kazi anazozifanya Dk.Samia na namna anavyoshuka chini kusilikiza kero za wananchi na kutatua.


"Kumbukumbu ziko vizuri hakuna asiyeijua kazi niliyoifanya nikiwa Chadema mwaka 2015 hadi 2017 niliwapiga kwa kupata viti vingi serikali za mitaa.Nawashukuru kwa kunipokea sasa niko tayari kuitumikia CCM .

Kwa upande wake Kishiwa amesema waliyokuwa wakiyapigania Rais Dk.Samia anaendelea kuyatatua na kuyafanyia kazi na hivyo anawashukuru wana CCM kwa kumpokea kundi na mjomba wake ushirikiano.


Akizungumza baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja 'Smart' amesema ;


" Nawapongeza wageni wetu waliojiunga nasi karibuni nyumbani, leo ninyi ni sawa na wana CCM wengine tuchape kazi."
Mbali na wanachama hao wawili mwingine pia kutoka Chadema alijiunga na CCM katika Shina namba 21 Kata ya Bujora wakiwemo wengine wapya zaidi ya 16.ssss
Aliyekuwa kuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Magu Mjini katika Wilaya ya Magu, Titus Gabriel (kulia), jana akipokea kadi ya uanachama kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa  Mwanza, baada ya kujiunga na CCM,Michael Masanja 'Smart'.
 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa  Mwanza, baada ya kujiunga na CCM,Michael Masanja 'Smart', akimvisha fulana ya CCM Titus Gabriel baada ya kujiengua kutoka CHADEMA jana.
 

Wanachama wapya waliojiunga na  CCM kutoka CHADEMA, titus Gabriel (kulia) na Said Kishiwa (kushoto) wakionyesha kadi zao za CCM muda mfupi baada ya kukabidhiwa. Picha na Baltazar Mashaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...