Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao wanayozalishwa nchini na usafirishaji.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Mkutano wa pili wa Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho "The Z Summit 2024" katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar tarehe: 21 Februari 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya ujenzi wa barabara mpya, kuboresha usambazaji wa umeme na maji pamoja na ujenzi wa viwanja vya ndege.

Halikadhalika, Rais Dk Mwinyi amesema Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar ya mwaka 2024 imeweka vivutio vingi ambavyo vinalinda uwekezaji na kuwa vivutio vya kodi Afrika Mashariki.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Pemba ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya baadae kwa kuanzishwa ukanda wa uwekezaji wa Pemba (PIZ) ili kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...