NA BALTAZAR MASHAKA, NYAMAGANA
MKUU wa Wilaya ya Nyamagana (DC),Amina Makilagi,amewataka wananchi wa Kata ya Mahina, waendelee kuiamini na kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo na huduma bora.
Pia, amewaonya wasiruhusu siasa kuigizwa katika miradi ya ya kijamii ya sekta za afya,elimu na miundombinu ya barabara wanayoletewa na serikali kuwa katika uchaguzi itakipaisha Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,mbunge na diwani, itaharibika.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia wananchi wa mitaa ya Igelegele na Kagomu,Kata ya Mahina wilayani Nyamagana,katika mkutano wa hadhara eneo la Mahina Kati.
Amesema imani huzaa imani,hivyo wananchi na jamii ya mahina waendelee kuiamini na kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita iwaletee maendeleo yatakayowawezesha kupata huduma bora.
“Nimekuja kuwaambia tumepokea mradi wa jengo la upasuaji katika Zahanati ya Mahina, ukikurupuka ukaanza bila kuwataarifu wenye mradi wakigoma utafanyaje.kazi yenu katika mradi huo mtachangia sh.milioni 11.9,serikali na mfadhili watawaunga mkono kwa sh.milioni 120,”ameeleza Makilagi.
Amesema mradi huo wa jengo upasuaji na jengo la wagonja wa nje (OPD) inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika zahanati hiyo ili kuwaepusha na vifo watoto na wajawazito,wazee pia watatibiwa hapo na hivyo wachangamkie fursa maana ni mradi wenu.
Mkuu huyo wa wilaya alisistiza mradi huo utawahudumia wananchi wote wana CCM,wa vyama vingine na wasio na vyama, hivyo wajitoe kuchangia na kushiriki ujenzi kwa kusaidia mafundi kusogeza mawe,matofali na kusomba maji si lazima wachangie fedha tu.
“Maendeleo yanaharibiwa na watu wenyewe na ninyi ndio mnafahamu adha mnayopata kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya,katika mradi huu mkiruhusu siasa ikaingizwa eti utampaisha Rais Samia katika uchaguzi, mtaukosa ama utaharibika,”amesema Makilangi na kuongeza;
“Atakayeingiza siasa au kuukwamisha mradi huu huyo ni size yangu na anayetaka kuiona rangi yangu ajaribu.Siku zote msaliti vitani au anayetoboa mtumbwi ili tuzame wote,huyo ni kumtosa safari iendelee.”
Naye mkazi wa Igelegele na mmoja wasimamizi wa mradi huo,Zihaya Khalid,ameeleza kuwa wanufaika wakubwa ni watoto na wajawazito wanaopata changamoto ya kujifungua kwa njia ya kawaida,hivyo atawaelimisha wananchi na jamii umuhimu na faida ya mradi.
“Sisi akinamama lazima tujivune kupata mradi huu sababu utakuwa na manufaa kwetu kuliko watu wengine.Wanaodhani hauna maslahi kwao nitawajibika kuwaelimisha na kuwahamasisha kujitolea tuukamilishe,”amesema.
Naye Mratibu wa TASAF Jiji la Mwanza, Peter Ngagani ameeleza kuwa serikali imewekeza sh.120,697,900, mchango wa jamii sh.11,969,500 ambapo mtaa wa Kagomu wenye kaya 1,788 kila moja itachanga sh.2,562 (4,580,000), kaya 2,238 za Igelegele sh.3,302 sawa na sh. 7,389,500.
Diwani wa Mahina (CCM) Alphonce Francis aliwaasa wananchi wa kata hiyo waiunge mkono serikali kutekeleza mradi huo wa jengo la upasuaji,wachangie asilimia 10 kama moja ya masharti ya mradi na wamwombee Rais Dk.Samia kwa dhamira njema ya kuwaletea maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, akihutubia wananchi wa Igelegele na Kagomu katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Mahina Kati kuhusu kupokea mradi wa upasuaji katika Zahanati ya Mahina.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kagomu, George Peche, leo akifungua mkutano wa hadhara kuhusu kupokewa kwa mradi wa jengo la upasuaji unaotekelezwa na TASAF katika Zahanati ya Mahina.
Diwani wa Mahina (CCM),, Alphonce Francis,leo akizungumza na wananchi wa mitaa ya Kagomu na Igelegele kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, katika mkutano huo ulioganyika Mahina Kati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...