Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amesema kuna haja ya watendaji wa kata kupewa elimu ya sheria mbalimbali zinazohusu raia ili waweze kutatua kesi na migogoro mbalimbali ya wananchi katika kata zao pasipo kumuonea.

Mwanziva ameyasema hayo katika hafla ya kilele cha siku ya sheria nchini ambapo wilayani humo ilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo huku akitoa agizo katika ofisi ya mwanasheria wa halmashauri kuhakikisha elimu hiyo inatilewa kabla ya mwezi frebruari kumalizika ili utatuzi wa haki katika migogoro ya wananchi uanze kutolewa.

Amesema sambamba na utoaji huo wa elimu kwa watendaji lakini wananchi pia wanapaswa kupatiwa elimu hiyo ili waweze kutambua haki zao kwakuwa wananchi walio wengi uelewa wao wa sheria bado ni mdogo kitu ambacho kinapelekea kujiona wanaonewa hata kwa jambo ambalo ni wakosaji.

Hata hivyo Mwanziva amempongeza Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo Isaac Ayeng'o kwa kuendesha mashauri kwa wakati pamoja na haki kwani tangu awasili katika wilaya hiyo hajawahi kupokea malalamiko juu yake kutoka kwa wananchi anaowapa huduma mahakamani hapo.

"Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza sana juu ya kupunguza mlolongo wa kesi mahakamani na kutoa haki kwa wahusika hivyo mahakama hii imekuwa ya mfano katika hili hivyo niwapongeze sana".









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...