WAZIRI wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Damas Ndumbaro amewapongeza washindi wa Tigo Marathoni huku akiongeza kuwa mafanikio yao yameakisi matayarisho mazuri waliyoyafanya kabla ya kushiriki kwao.
Akizungumza katika mashindano hayo alisema kuwa ushindi huu ukawe chachu kwa wengine kujiandaa vyema ili mwakani wafanye vizuri na kujituma zaidi ili kulinda mafanikio waliyoyapata.
Pia aliwapongeza wandaaji wa mbio hizo kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na chama cha riadha duniani (World Athletics) na kila cha hapa nchini (RT) kwa michango yao iliyochangia Kilimanjaro Marathon iendelee kuwa maarufu.
Katika hizo, mshindi kwa upande wa wanaume Watanzania wakiongozwa na Faraja Lazaro Damas walishika nafasi tisa kati ya nafasi kumi bora isipokuwa nafasi ya pili iliyoshikwa na Mkenya Peter Mwangi ambapo Damas alitumia muda wa saa 1:03:33 hii y Mwangi aliyetumia muda wa saa 1:03:44.
Akizungumza mara baada ya kuibuka kidedea katika Mbio za Tigo International Half Marathon 2024, Damas kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alimshukuru Mungu kwa ushindi huo pamoja na wadhamini wa mashindano hayo Kampuni ya Tigo kwa kumsaidia kutimiza malengo na ndoto zake za kuwa Mwanariadha mkubwa nchini atakefuzu na kushinda mashindano mbalimbali duniani na kuliletea taifa Medali mbalimbali za Kimataifa.
"Ninamshukuru sana Mungu kwa kipaji alichonijalia kwani kasi ipo kwangu na kasi ipo Tigo 4G na ninaamini kuwa nitakwenda kuiwakilisha Tanzania vyema mwezi Aprili mwaka huu Viena katika kufuzu kushiriki mashindano ya Olympiki yanayotarajiwa kufanyika katika jiji la Paris nchini Ufaransa mwezi Agosti mwaka huu," alifafanua Damas kwa bashasha.
Kwa upande wa wanawake, Wanaraiadaha wa Taznania pia wameng'ra katika Mbio hizo ambapo Failuna Abdi Matanga aliongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa 1:16:54 akifuatiwa na Mtanzania mwenzake Neema Kisuda aliyeshika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa 1:16:54.
Akizungumza katika Mbio hizo, Afisa Mkuu wa Fedha wa kampuni ya Tigo, Innocent Rwetabura alifafanua kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini Mbio za Tigo International Kili Half Marathon(mwaka wa 9 sasa) moja ya mbio za Kilimanjaro International Marathon ambazo zimefikisha miaka 22 yenye mafanikio makubwa.
"Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza waandaji wa mbio hizi kwa kuendesha mbio hizi kwa weledi mkubwa na kuzifanya kuwa za viwango vya kimataifa." alifafanua afisa huyo na kuongeza kuwa;
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...