SHIRIKA la AMEND Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi nchini wameendelea na mradi wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda katika Jiji la Tanga ambapo elimu hiyo imetolewa kwa madereva bodaboda wa kituo cha Shakamai katika Kata ya Magaoni.

Lengo la kutolewa kwa elimu hiyo kwa madereva bodaboda ni kuhakikisha wanapokuwa barabarani wanazingatia sheria za usalama barabarani sambamba na kupata elimu ya kutoa huduma ya kwanza iwapo itatokea ajali kwa dereva wa bodaboda au abiria.

Baadhi ya madereva wa bodaboda wa jijini Tanga wakielezea elimu walioipata wameeleza kwamba itawasaidia kujiokoa wao wenyewe pamoja na kuokoa maisha ya watu wengine wanapokuwa barabarani.

Aidha wamesema kuwa kabla ya kupata mafunzo hayo baadhi ya madereva bodaboda wamepoteza maisha na wengine kubaki na ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kukosa elimu ya huduma ya kwanza.

Wamesisitiza sababu zinazopelekea ajali kwa madereva bodaboda ni pamoja na kutozingatia alama za barabarani pamoja na mwendokasi huku wakiendelea kuww elimu walioipata itawasaidia kuwa katika hali ya usalama zaidi.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo ya usalama barabarani Ofisa Miradi wa AMEND Ramadhani Nyanza amesema mradi wa elimu ya usalama barabarani kwa madereva bodaboda lengo lake ni kuwajengea uelewa kuhusu namna bora ya kuwa salama pindi wanapokuwa barabarani.

Ameongeza pia wanatoa elimu kwa madereva hao namna bora ya kutoa huduma ya kwanza pale ajali inapotokea huku akifafanua katika kufanikisha elimu hiyo wameshirikiana na Ubalozi wa Uswisi na kwamba katika Jiji la Tanga wanatatajia madereva wa maeneo mbalimbali wa Jiji hilo.

"Mafunzo ya usalama barabarani yanatolewa bila malipo kwa madereva bodaboda hivyo ametoa wito kwa madereva hao kushiriki kwenye mafunzo hayo jambo litakalowasaidia kuwa na uelewa kuhusu usalama wao wakati wanapokuwa barabarani, " amesema Nyanza na kusisitiza kuwa elimu hiyo wanatarajia kuitoa katika vijiwe mbalimbali vya bodaboda jijini Tanga.

Dereva bodaboda Othman Juma na John Muhina wametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo wamefurahishwa na mradi huo wa kuwapatia elimu na kwamba wanaamini kuanzia sasa watakuwa mabalozi wazuri wa kuifikisha elimu hiyo kwa wenzao ambao bado hawajaipata.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...