NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu (MCC), Mohammed Ally Kawaida amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani itaendelea kuboresha mazingira kwa Vijana ili waweze kujiajiri wenyewe na kukabiliana na changamoto ya Ajira nchini.

Kawaida ametoa kauli hiyo alipotembelea kikundi cha Vijana kinachojishughulisha na uchapishaji cha Quality Printing Press kilichopo Moshi mjini mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, lengo la serikali ni kutengeneza mazingira rafiki kwa Vijana kujiajiri.

Alisema kuwa, katika kuhakikisha lengo hilo linatimia Serikali itaendelea kutoa mikopo kwa Vijana kama mitaji ya kuanzisha biashara mbalimbali.

"Lengo la serikali ni kumaliza tatizo la Ajira kwa Vijana ndio maana ilikuja na mradi wa Jengo kesho iliyo bora (BBT) ambapo Vijana walipatiwa elimu ya maswala ya Kilimo pamoja na kupatiwa mashamba yenye miundombinu yote ya Kilimo pamoja na mitaji" Alisema Mwenyekiti Kawaida.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu alisema kuwa, katika kuhakikisha Vijana wanatengenezewa mazingira rafiki ya kuanzisha viwanda ili waweze kujiajiri na kwamba serikali imeendelea kuboresha swala la upatikanaji wa umeme wa uhakika.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...