Kikao kazi cha Nne cha Wadau wa Huduma za Serikali Mtandao ( e-GA ) kimehitimishwa tarehe 08 Februari,2024 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika tukio hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza Waandaaji kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika siku 4 za kikao hicho na kuzitaka Taasisi za Umma kuongeza matumizi ya Serikali Mtandao katika Huduma zake.
Awali Mheshimiwa Naibu Waziri Kikwete alitembelea Mabanda mbalimbali ya maonesho ya Wadau wa huduma za Serikali Mtandao ambapo katika Banda la TPA ametoa pongezi kwa Mamlaka hiyo kufuatia kuanza kutumika kwa mfumo wa pamoja wa Kielektroniki wa uondoshaji wa Shehena Bandarini “ Single Window System “ unaoiunganisha TPA na Mamlaka nyingine zinazohusika katika mnyororo wa Huduma za Kibandari.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...