NA WILLIUM PAUL.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt.Festo Dugange amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro kutenga fedha za mapato kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya Umbwe.

Mbali na hilo amemwagiza pia amemwagiza kutumia fedha za vifaa tiba kwa ajili ya kununulia majokovu ya jengo hilo ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Hayo yamekuja baada ya Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwa kuishukuru Serikali kwa kuwapatia gari la kubebea wagonjwa ambalo wamelipeleka katika kituo cha Afya Umbwe.

Prof. Ndakidemi alisema kuwa, kituo hicho cha Afya kinahudumia kata 6 katika Tarafa ya Kibosho lakini hakina chumba cha kuhifadhia maiti (Mortuary) je Serikali inampango gani kuwasaidia kuwajengea jengo la kuhifadhia maiti katika kituo hicho.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Dkt. Festo Dugange alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Wabunge kwa kupokea magari ya kubebea Wagonjwa ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani ameyanunua kwa ajili ya majimbo yote na Halmashauri nchini.

Dkt. Dugange alisema kuwa, wanaendelea kuboresha huduma za kuhifadhi maiti (Mortuary) na kutumia nafasi hiyo kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi kutenga fedha za mapato ya ndani kujenga jengo hilo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...