Imebainishwa kuwa upungufu wa damu unaosababishwa na lishe duni umetajwa kuwa chanzo vya vifo vya mama na mtoto visiwani Zanzibar. 

mkutano wa wadau wa lishe ulioandaliwa na taasisi ya maisha bora – ZMBF inayotekeleza mradi wa lishe. Mkurugenzi wa kinga na elimu ya afya wa wizara ya Afya Zanzibar, DKT. SALIM SLIM Amesema tathmini iliyofanywa na Wizara hiyo imebaini asilimia 65.9 ya wanawake na watoto Zanzibar wana tatizo la lishe duni na upungufu wa damu hali inayo sababisha vifo vya uzazi.

Mradi wa lishe unaotekelezwa kwa ushirikiano wa ZMBF, taasisi ya BENJAMIN MKAPA na wadau wa lishe umeendelea kuhamasisha lishe bora kwa kwa kutoa elimu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na pia kuwafikia zaidi ya wananchi ELFU ISHIRINI NA SITA visiwani Zanzibar.

Naibu waziri wa afya Zanzibar HASSAN KHAMIS HAFIDH na mjumbe wa bodi wa ZMBF na naibu spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar MGENI HASSAN JUMA wamesema kuna haja serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kuongeza bajeti ya lishe ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto.

Mwenyekiti wa taasi ya maisha bora na mke wa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mama MARIAM MWINYI ameishauri wizara ya afya Zanzibar kuunda kamati ya lishe ya taifa ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo.

ZMBF Imetoa vitendea kazi mbalimbali kwa wahudumu TISINI wa afya ngazi ya jamii wa visiwa vya PEMBA na UNGUJA ili wawafikie wananchi kwa urahisi







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...