Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imetoa ahirisho la mwisho katika kesi ya kujeruhi inayomkabili mfanyakazi wa benki ya CRDB , Ibrahim Masahi anayetuhumiwa kumpiga na nyundo jirani yake Deogratus Minja baada ya kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa kutokana na mashahidi kutokufika mahakamani.
Wakili wa Serikali, Salma Jafari amedai leo mbele ya Hakimu Mkazi, Amos Rweikiza kuwa kesi ililetwa kwa ajili ya usikilizwaji, lakini hawezi kuendelea kwa sababu hawana shahidi, shahidi ambae walimtegemea amepata udhulu, kwa hiyo wanaiomba mahakama ipange tarehe nyingine.
Hakimu Rweikiza, akamuuliza Wakili wa utetezi, Nestory Wandiba kama amesikia kilicozungumzwa na Jafari, "Sina pingamizi kwa hicho, lakini hii ni mara ya pili upande wa Jamhuri unasema hauna shahidi kama nakumbuka mara ya mwisho kusikiliza kesi hii ilikuwa ni Desemba 12,2023, nawaomba wajitaidi kuleta mashahidi wao la sivyo wafunge," amedai Wandiba
"Umesikia wakili haya yaliyozungumzwa kesi hii ni ya muda mrefu na huyu ni mtumishi anatakiwa awepo kazini, kesi hii ni ya tangu mwezi Machi inatakiwa kuisha, sasa natoa ahirisho la mwisho Februari 27,2024 lazima mlete shahidi," amesema Hakimu Rweikiza
Awali, Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kitendo cha Mifupa (MOI), Joel Mwinza (44), aliieleza Mahakama jinsi alivyomtibu Minja aliyedaiwa kushambuliwa na nyundo na Masahi, alimpokea akiwa na
majeraha kichwani, mgongoni, mkononi na pia kuna sehemu alikuwa amechanika kisogoni, kwa hiyo alitumia mashine ya X-ray na CT Scan kumchunguza mwili wake.
Katika ushahidi wake, Minja amedai kuwa tarehe hiyo saa mbili na nusu usiku alikuwa akipita nje ya geti la jirani yake Masahi, alimkuta kijana wa jirani huyo, baada ya kumuona alizungumza kwa kilugha kwa sauti kubwa ambae yeye hakuielewa.
"Ghafla kijana alikuja mbele yangu akanizuia nisipite, mara geti likafunguliwa akatoka Masahi akanihoji kwamba mimi ni kama nani na kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa, sikumjibu chochote kijana wake akanipiga ngumi,"
"Nilimgeukia jirani yangu ili amuonye kijana wake, lakini na yeye aliinua shati lake akatoa nyundo akanipiga nayo kichwani baada ya kupata maumivu makali nilianza kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada,"amedai Minja.
Amedai kuwa, alianguka chini ndipo Masahi akaanza tena kumshambulia na nyundo mgongoni, maumivu yalipomzidi aligeuka, akampiga na nyundo kwenye mkono wa kulia na kwenye bega.
Jirani mmoja alifungua geti na kumsaidia kwa sababu alikuwa ana kuja damu nyingi walimpeleka Hospitali ya Bochi kwa matibabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...