Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MCHEZAJI mpya wa timu ya soka ua Simba ya jijini Dar es Salaam PA JOBE amesema kuwa hajaja katika timu kufanya holiday bali amekuja Tanzania kufanya kazi.

PA JOBE ameyasema hayo baada ya kufunga goli lake la kwanza dhidi ya Timu ya Tembo FC ya mkoani Tabora katika mchezo uliochezwa uwanja wa Azam uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam

"Sijaja holiday nimekuja hapa kufanya kazi, ingekuwa holiday ningebaki Ulaya kula Bata, nimecheza Ulaya na kucheza Ulaya ni rahisi kuliko kucheza Afrika, siko hapa kucheza pasi kufurahisha, nipo hapa kufunga, " amesema.

Amesema kwamba watu wana wasiwasi na yeye, hawamuamini lakini hilo hajali na anataka kuwaonyesha." Msimu uliopita Ulaya nilifunga mabao 30 nataka niwaprove wrong (kuwathibitishia).

"Sijafurahia na kiwango nilichokionyesha leo kwa sababu nimepata nafasi na nimepiga nje, straika unapokosa nafasi inaumiza, " amesema PA JOBE ambaye alikuwa akizungumza kwa kujiamini kuhusu uwezo wake uwanjani.

"Kuhusu Simba unajua ni klabu kubwa Afrika, kabla ya kuja hapa naijua na kabla sijaenda Ulaya nimecheza Champions league nikiwa Algeria nina uzoefu". Ameongea straika mpya wa Simba Pa Omary Jobe ambaye hapo jana alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...