Na JANETH RAPHAEL - MichuziTv

Imeelezwa kuwa mfumuko mkubwa wa bei katika bidhaa Mbalimbali nchini unaathiri uchumi na kupunguza uwezo wa wananchi kununua bidhaa na huduma hizo hivyo kuadhiri hali halisi za maisha.

Mchumi toka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) John mero ametoa kauli hiyo Leo wakati wa semina iliyoandaliwa na BOT Unguja Zanzibar katika ofisi ndogo za makao makuu ya benki hiyo

Mero amesema mfumuko huo wa bei pia hupunguza uwezo wa akiba waliyonayo ya kununua bidhaa na huduma na kupunguza uwekezaji na kufifisha mizunguko wa fedha nchini.

"Benki Kuu zimepewa jukumu la kudhibiti mfumuko wa bei kwa kuwa ndiyo Taasisi pekee zinazotoa fedha na kuwa na uwezo wa kudhibiti mizunguko wa uchumi" amesema Mero 

Mchumi huyo pia amesema utekelezaji wa fedha unalenga utulivu wa bei za bidhaa na huduma na kuwezesha shughuli za Uchumi.

Hata hivyo amesema tafiti zinazonyesha kuwa chanzo kikubwa cha mfumuko wa bei ni ongezeko la ujazi wa fedha usioendana na hali ya shughuli za Uchumi.

Hata hivyo amesema tafiti zinazonyesha kuwa chanzo kikubwa cha mfumuko wa bei ni ongezeko la ujazi wa fedha usioendana na hali ya shughuli za Uchumi.

Semina hiyo ya siku tatu imefunghuliwa leo Februari 14, 2024 na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandambila.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...