Na Mwandishi wetu - Ruvuma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama ametoa wito viongozi kuhakikisha wanawapatia wenyeviti wa Mashina wa Chama cha Mapinduzi taarifa muhimu za utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ili waweze kuzielezea vyema kwa Wananchi.

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo Wakati wa ziara yake ya kutembelea Wenyeviti wa Mashina Katika Kata ya Magagula;Mbingamwalule, Kizuka, Liganga, na Litisha zilizopo Jimbo la Peramiho lilopo katika Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Ameongeza kusema kwamba siasa za sasa zinalenga katika kujenga hoja hivyo ni muhimu wenyeviti wa Mashina kuwa na maelezo muhimu yatakayosaidia kukielezea Chama vyema kwa wananchi.

"Utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM inategemea Mafiga Matatu kwa maana ya Rais, Mbunge na Diwani Jambo ambalo linarahisisha katika utekelezaji wa shughuli za serikali na heshima hiyo mnatupatia nyie wenyeviti wa Mashina," alisema.

Aliongezea kuwa Wenyeviti mwendelee kuwa na uelewa mzuri wa miradi inayotekelezwa na Serikali kwani itasaidia kusemea Chama, na Rais ikiwa ni sambamba na kusaidia kusukuma Gurudumu la maendeleo pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Thomas Masolwa amesema ziara ya Mhagama kutembelea Wenyeviti Mashina inasaidia kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Ameongeza kusema kuelekea uchaguzi ujao ni vyema Wenyeviti wa Mashina wakajua kwamba Uchaguzi ni hesabu za namba, ukiwa na namba nyingi lazima utakuwa umemshinda mpinzani wako.

" Ni vyema tuhamasishe wananchi waende kukipiga Kura Chama Cha Mapinduzi, tutengeneze wapiga Kura kwa kuhakikisha wanasajiliwa ili watambulike na Chama," alisema.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...