Na; Mwandishi Wetu - Dodoma

Serikali imepanga kufanya tathmini ya mafunzo yanayotolewa kupitia programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25 ili kujiridhisha na ubora wa mafunzo hayo.

Amesema hayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajura na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi leo Februari 7, 2024 bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Latifa Juakali, Mbunge wa Viti Maalum, ambaye amehoji, ni kwa kiasi gani Serikali imefanya tathmini ya mafunzo wanayopatiwa vijana nchini kupitia ofisi hiyo baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Aidha, Mhe. Katambi amesema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 serikali ilifanya utafiti wa nguvukazi ambapo kiwango cha Ujuzi cha chini kimeanza kuboreka.

Vile vile, Mhe. Katambi amesema kuwa, Serikali imeendelea kuwezesha vijana kupitia programu mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na changamoto ya ajira.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akijibu swali  bungeni leo tarehe 7 Februari, 2024, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...