MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imezindua rasmi mpango wa kuendeleza watalaam ambao wamethibitishwa katika sekta ya masoko ya mitaji ambao watatakiwa kila mwaka kukidhi matakwa ya angalau kuwa na saa 35 ya kuwawezesha kuwa utalaam ambao ni endelevu na wa kisasa zaidi ili kuhakikisha wanatoa bidhaa mpya na bunifu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Warsha ya wadau wa masoko ya mitaji kuhusu utekelezaji wa mpango wa maendeleo na uzinduzi wa mafunzo endelevu kwa watalaam wa sekta hiyo,Kamishina wa Uendelezaji Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Charles Mwamwaja amesema nchi yetu kwa sasa imepiga hatua kubwa kwa maana ya miongozo ya kisera ,sheria na taratibu zinazowezesha matumizi masoko ya mitaji

“Masoko ya mitaji ni masoko kama yalivyo masoko mengine lakini yanatoa fursa ya watu wanaohitaji mitaji mbalimbali kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo .Sasa ipo namna ambavyo mitaji hii inapatikana na kama nilivyosema Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imejenga mazingira mazuri kiasi cha kuifanya Tanzania kuwa ni moja ya nchi za kupigiwa mfano katika ukanda huu wa Afrika katika kuongoza katika matumizi ya haya masoko ya mitaji

“Hivi karibuni mmeshuhudia Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa katika kutoa hatifungani mbalimbali katika masoko ya mitaji mbalimbali.Mtakumbuka hivi karibuni Benki ya CRDB hatifungani ya kijani ambayo iliweza kupata fedha nyingi kwa wakati mmoja lakini pia hata benki ya NMB na wadau wengine

“Wiki iliyopita pale jijini Tanga tulikuwa na tukio lingine ambalo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.Tumefanya uzinduzi wa hatifungani ya kijani ambayo ilitolewa na Mamlaka ya Maji yaani TANGAWASA.Sasa matumizi haya ya hatifungani kwenye kupata mitaji ya kutengeneza miradi ya maendeleo tunahitaji matumizi ya njia mbadala,”amesema.

Amefafanua ni njia ambayo tofauti za zile ambazo zimekuwa zikitumika siku zote kwa maana ya kwamba wadau wote wamekuwa wakiitegemea bajeti ya Serikali wakati ziko fursa za kutumia masoko hayo ili baadhi ya miradi ya maendeleo itekelezwe kwa utaratibu huo.

“Kubwa ambalo tunalifanya leo tunazindua mpango maalum ambao utawezesha kuendelea kuwajenga uwezo na uelewa watalaam wetu katika sekta hii ya masoko ya mitaji ili miradi miradi yetu iandaliwe kwa viwango fulani vya kitaalam.

“Kuna viwango vya kitaalam na taaluma inayohitajika ili miradi hii iweze kukidhi vigezo na kukubalika katika masoko haya ya ndani. Kwa hiyo tunaowatalaamu wetu wa ndani , tunaoutaratibu wa kuwajenga uwezo na tukasema utaratibu wa kuwajenga uwezo uwe ni kila mwaka.

Kwa hiyo kundi kubwa lililopo hapa leo limekuja kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo haya ili sasa miradi yetu tunayoitengeneza iwe bora na yenye kukidhi viwango vinavyokubalika kimataifa.“Kwahiyo wapo hapa watalaamu wetu wanapikwa na kwa muda mfupi Tanzania itaendelea kuwa eneo muhimu na la kupigiwa mfano na wadau wengi watakuja kujifunza kwenye masoko haya ya mitaji katika kutekeleza hiyo miradi yao.”

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) CPA.Nicodemus Mkama amesema wamekutana na wadau wa masoko ya mitaji na dhamana kufanya tathimini ya utekelezaji wa mpango wa miaka 10 ya uendelezaji wa sekta ya fedha nchini katika sekta ya masoko na mitaji

Amesema tathimini imefanyika na kuona sekta ya masoko ya mitaji imetekeleza kwa ufanisi malengo yaliyowekwa katika mpango mkuu wa uendelezaji sekta ya fedha kwani katika kipindi cha miaka mitatu wa mpango huu mengi yametekelezwa kwa mafanikio makuwa.

“Mpango huu ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2020/2021 na utamalizika mwaka wa fedha 2029/2030.Mpaka sasa tumeweza kuongeza thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kwa asilimia 31.2 na kufikia Sh. trilioni 37.2

“Mauzo katika soko la hisa Dar es Salaam yameongezeka kwa asilimia 61.8 kufikia Sh. trilioni 9.3 kwa hiyo haya ni mafanikio makubwa yamepatikana katika kipindi cha utekelezaji wa mpango wa uendelezaji sekta ya fedha

“Pia kulikuwa na bidhaa mpya za ubunifu zimetolewa katika masoko yetu ya mitaji ikiwa na hatifungani ya kijani iliyotolewa na Benki ya CRDB na kupata mafanikio makubwa lakini vile vile hatifungani ya maendeleo ya jamii zilizotolewa na Benki ya NMB.Hatifungani ya TANGA UWASA ambapo tunatarajia kupata fedha takriban Sh.bilioni 53.2 kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya sekta ya maji lakini utunzaji wa mazingira.

“Hatifungani hizi zimeweza kufanya vizuri sana katika ukanda wa Kusini mwa Afrika na hivyo kufikia matarajio ambayo yamewekwa katika mpango mkuu.Siri ya mafanikio ya mpango huu ni kutokana na mazingira wezeshi pamoja na shirikishi yanayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na kuwezesha kupatikana kwa mafanikio haya.”

Amesisitiza pamoja na hayo leo wanazindua mpango wa watalaam ambao wamethibitishwa katika sekta ya masoko ya mitaji ambao sasa watatakiwa kila mwaka kukidhi matakwa ya angalau kuwa na saa 35 ya kuwawezesha kuwa utalaam ambao ni endelevu na wa kisasa zaidi ili kuhakikisha tunatoa bidhaa mpya na bunifu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...