-Ni kutokana na mchango wake kwenye kusimamia sekta ya ushirika nchini.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itamkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tabora na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Hassan Wakasuvi kutokana na mchango wake mkubwa katika shughuli za maendeleo nchini.

Amesema hayo leo (Jumamosi Februari 24, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maziko ya Ndugu Wakasuvi yaliyofanyika katika kijiji cha Mabama mkoani Tabora.

Amesema kuwa Ndugu Wakasuvi alikuwa kiongozi imara katika kusimamia shughuli za maendeleo ikiwemo sekta ushirika nchini na umahiri wake uliwezesha kuimarika kwa sekta hiyo na kuleta tija nchini. “Aliiwakilisha nchi vyema kwenye sekta ya ushirika sio Tanzania tu, bali Afrika Mashariki, Ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Afrika kwa ujumla. ”

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi amesema Ndugu Wakasuvi alikuwa na kiwango kikubwa cha kuaminika.

Ameongeza kuwa Ndugu Wakasuvi alikuwa kinara katika kuchochea umoja ndani ya CCM pamoja na maendeleo ndani ya nchi. Leo "Chama, Serikali na Wananchi tumepoteza kiongozi mahiri, tumuenzi kwa kuendeleza umoja na mshikamano.”






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...