Na Janeth Raphael MichuziTv - DODOMA.

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mh Ummy Ndelianga ameihimiza Wizara, Wakala,Mamlaka,Taasisi,Maahirika ya Umma na wadau wote wanaotekeleza afua za lishe kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kutoa taarifa sahihi na fasaha katika zoezi la utafiti wa gharama za Utapiamlo ili kupata matokeo yenye tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.

NAIBU Waziri Ndelianga ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma katika uzinduzi Rasmi wa zoezi la Utafiti wa gharama za Utapiamlo Nchini,uliofanyika katika Ofisi zao.

Na kuongeza kuwa wawe tayari kutoa muda na ruksa watalaamu wao ili kushiriki kikamilifu katika Kazi ya timu ya Taifa ya utafiti.

"Ndugu Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Sisi kama Serikali tunasubiri kwa hamu matokeo ya zoezi hili kwani yatatumika kuongeza uelewa miongoni mwa watendaji, watunga sera na waweka mipango kuhusu athari za utapiamlo".

"Katika kuhitimisha hotuba yangu naomba kusisitiza mambo yafuatayo; Wizara, Wakala, Mamlaka, Taasisi, Mashirika ya Umma na wadau wote wanaotekeleza afua za lishe kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kutoa taarifa sahihi na fasaha ili kupata matokea yenye tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla;Wizara, Wakala, Mamlaka, Taasisi na Mashirika ya umma kuwa tayari kutoa muda na ruhusa kwa wataalamu wao ili kishikiki kikamilifu katika kazi za Timu ya Taifa ya Utafiti (National Implementation Team);Timu ya Taifa ya Utafiti ifanye kazi zake kwa uadilifu na kwa kuzingatia mpango kazi wake; naIdara ya Uratibu iliyo Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha kutoa taarifa za mara kwa mara Serikalini kuhusu hatua za utekelezaji wa zoezi hili".

Aidha amesema kuwa ameridhishwa na taarifa zote zilizotolewa pamoja na msingi wa umuhimu wa zoezi hili.

"Kwa ujumla nimeridhika na taarifa zote mlizotupatia kuhusu chimbuko, msingi na umuhimu wa kufanya zoezi la utafiti huu pamoja na maelezo ya jinsi mlivyojipanga kulitekeleza. Vilevile, nimefarijika kwa maelezo mliyoyatoa kuhusu mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha kuwa pengo la bajeti kutokana na changamoto ya upatikanaji wa rasilimali fedha linafanyiwa kazi na ni matumaini yangu kuwa fedha hizi zitapatikana kwa wakati ili zoezi lisikwame na likamilike kwa ufanisi.

Kipekee ninapenda kuwashukuru wataalamu wa Chakula na Lishe kwa kuishauri vyema Serikali juu ya umuhimu wa utafiti huu katika nchi yetu tunapokwenda kuandaa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Pia niwashukuru wadau wetu wakiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) ambao tayari wameshatoa fedha ambazo zitasaidia sana katika hatua muhimu za utafiti huu.

Aidha, katika hadhara hii nimesikia kuwa wapo wadau wengine kama vile USAID Tanzania, FAO, Irish Embassy, Hellen Keller International – HKI na SANKU ambao tumekuwa tukishirikiana nao katika masuala mbalimbali ya lishe nchini.

Basi niwaombe nao waone umuhimu wa utafiti huu na kuweka mikakati ya kuziba pengo la raslimali fedha lililopo ili kukamilisha kazi hii kwa wakati. Pia niwakaribishe wadau wengine wote wenye mapenzi mema katika kuunga mkono juhudi za kuboresha na kuimarisha Lishe zinazoongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".

Naye mwakilishi kutoka Zanzibar Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa pili wa Raisi Zanzibar Ndugu Salhina Mwita amesema kuwa katika hili la utafiti tutashirikiana kwa pamoja kabisa ili kufikia malengo kusudiwa.

"Mh Naibu Waziri kwa upande wa Zanzibar,Mimi na kwa niaba ya wenzangu tutashirikiana kwa pamoja kabisa,tukiwa na tunaamini matokeo ya Utafiti huu yatatupeleka kwenye yale maeneo yaliyokusudiwa na malengo yetu ya baadae".

Kwa upande wake mwakilishi kutoka UNICEF Bwana John George amesema kuwa takwimu zikipatikana zaidi wanaweza kufanya Kazi na kushawishi zaidi.

"Tukipata takwimu zaidi naamini tunaweza kufanya Kazi na kushawishi zaidi kwaajili ya kuzuia utapiamlo"."Kwahiyo tunapenda kuona miaka mitano ijayo hali Inakuwa safi zaidi na kiwango kikiendelea kupungua".

Zoezi hili ni moja Kati ya Shughuli zinazoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...