Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

VIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali ya dini pamoja na wajasiriamali katika Mkoa wa Kilimanjaro wamepatiwa bure mitungi ya gesi ya Oryx 1000 pamoja na majiko yake kwa lengo la kulihusisha kundi hilo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.

Mitungi hiyo ya gesi ya Oryx na majiko yake imetolewa kwa viongozi hao wa dini na Kampuni ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond  ikiwa ni sehemu ya mipango na mikakati ya kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukagwa mitungi hiyo kwa viongozi wa dini na wajasriamali wa mkoa huo, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ametumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa dini kutumia nafasi zao kujikita pia katika kusaidia jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuachana kutumia kuni na mkaa.

“Unaweza kutafakari na kujiuliza kwanini Mbunge Shally Raymond na Kampuni ya Oryx wameamua kuwaita viongozi wa dini kuhamasisha utunzaji mazingira?Ni kwasababu viongozi wa dini  ni watu wa thamani sana , unajua sisi binadamu watu ambao tunawathamini na kuwasikiliza ni viongozi wetu wa dini na mimi kwa utashi wangu mdogo naamini tunawasikiliza viongozi wa dini kwasababu kazi ya kueneza neno la Mungu hakuna anayelipwa.

“Kwa maana hiyo ndio maana mama Shally pamoja na makundi mengine yote aliamua kuleta viongozi wa dini kwakuwa sisi tunawaheshimu ,tuna matumaini makubwa na viongozi wa dini.Tunaamini  viongozi wa dini ndio ambao wanaweza kutusaidia kuwaelimisha na kuwaambia wananchi kuhusu kutunza mazingira,”amesema Naibu Waziri Kapinga

Amesisitiza kwa watu wengine ambao huna sura ya kimungu ni ngumu kuaminika lakini akisema kiongozi wa dini msikate miti watu wanaamini huyu ametumwa na Mungu hatutaka miti, akituambia tuache kutumia kuni,tuache kutumia mkaa kwasababu tunazidi kukata miti tunazidi kuleta mabadiliko ya tabianchi.

Ameongeza kuwa uharibifu wa mazingira unatokana na ukataji miti imessababisha hata mikoa iliyokuwa na mvua nyingi kama mikoa ya nyanda za juu kusini ambazo zilitakiwa mvua kuanza Novemba zinaanza mwishoni mwa Desemba

“Kwanini kwasababu ya matendo yetu wenyewe ya kuharibu mazingira.Kwahiyo tunaamini viongozi wa dini mpo katika nafasi ya kutusaidia kuendelea kukumbusha jamii kwamba dunia hii ambayo tumepewa zawadi na Mwenyezi Mungu ni haki ya kila mmoja kuilinda leo, tunawatoto na wajukuu na tutakuwa na vitukuu pia, ssa kama rasilimali zote tulizonazo tutazichezea leo hawa wajuu na vitukuu vitaishi katika mazingira gani”

Amesema ni vema kuendelea kulinda mazingira yetu kwa ajili ya wengine na kuwahusisha viongozi wa dini ni muhimu kwasababu ni kundi ambalo linasikilizwa na hivyo amewaomba kusaidia katika ajenda hiyo ya nishati safi ya kupikia

Pia amesema kuwa katika kampeni hiyo ya kuhamasisha matumizi ya nishati ya kupikia wamekuwa wakihusisha zaidi wanwake kwasababu wanawake ndio wanaokaa jikoni kupika kuandaa chakula.“Kwahiyo mwaka 2024 tusikubali kupika kwa kuni wala mkaa.

“TUnawashukuru Oryx kwa kutupatia majiko ya gesi lakini njia za nishati safi ya kupikia ni ile tu kasumba kwamba hii ni gharama lakini ndugu zangu kibaba cha mkaa wa Sh.2000 jioni hakifiki.Ni gharama nafuu kutumia nishati safi kuliko kutumia kuni na mkaa katika kuandaa chakula.”

Aidha amesema pamoja na uwepo wa changamoto zinazotokana uharibifu wa mazingira bado kuna fursa kwa jamii kujirekebisha kwa kulinda mazingira.

Akizungumzia kampeni ya nishati safi ya kupikia, Naibu Waziri Kapinga amesema mwaka jana mwishoni kulikuwa kuna mkutano wa dunia wa mazingira na katika mkutano huo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alienda na ajenda mahususi ya kumkomboa mwanamke wa Afrika sio mwanamke wa Tanzania peke yake.

“Kumkomboa vipi?Kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawake wote wa Afrika wanatumia nishati safi ya kupikia na katika mkutano ule ulihusisha wakuu wa nchii. Rais Dk.Samia kutokana na umahiri wake na uwezo wake aliweza kukusanya viongozi na kuzindua program maalum kusaidia wanawake wa Afrika kwenye kutumia nishati safi ya kupikia.

“Kwa hiyo ndgu zangu tunapozungumzia nishati safi ya kupikia tunazungumzia mambo ambayo yamebebwa ndani ya moyo wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ni ajenda yake ambayo yeye mwenyewe ameibeba. Tunapozungumzia wanawake wa Afrika tunazungumzia na wanawake wa Tanzania ,kwa hiyo kwa lugha nyepesi sisi wanawake wa Tanzania ndio wabeba bendera wa kumsaidia Rais kwenye ajenda hii ya nishati safi ya kupikia ili tuwe mfano kwa mataifa mengine,”amesema.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.

“Kufanya hivyo tunaamini tunaikomboa jamiina taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kueuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa.Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni,”amesema Fundi.

Amesisiza kampuni hiyo kwa kutambua nafasi ya viongozi wa dini imeona ni vema sasa ikatoa mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake kwa kundi hilo sambamba na kuelezea kwa kina umuhimu wa kutunza mazingira na wanaamini kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusema na kusikilizwa, hivyo watakapokuwa mabalozi wa kuzungumzia nishati safi ya kupikia jamii itabadilika na hivyo kuokoa mazingira.

Aidha amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032  asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa ya mitungi 19000 bure yenye thamani isiyopungua Sh.bilioni 1.5.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la  Moshi Mjini Priscus Tarimo( wa kwanza kushoto) Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond( wa pili kushoto) Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Kilimanjaro( wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi( wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya oryx Sister Piala Olomi kutoka Shirika la Masisita wa Bibi Yetu mkoa wa Kilimanjaro wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la  Moshi Mjini Priscus Tarimo( wa kwanza kushoto),  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Kilimanjaro ( wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi( wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Ofisa Daawa Manispaa ya Moshi Shekhe Hashim Mmbaga wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.Aliyeshika kipaza sauti ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond( wa pili kushoto). Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( mwenye nguo nyeupe) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro( wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi( wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Mwenyekiti wa Kanda ya Sita KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Kyomu mkoani Kilimanjaro Mchungaji Fredrick Minja wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.Aliyeshika kipaza sauti ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond( wa pili kushoto). 
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la  Moshi Mjini Priscus Tarimo( wa kwanza kushoto),Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond( wa pili kushoto) Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Kilimanjaro( wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi( wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Ofisa Daawa wa Kata ya Msaranga iliyopo Moshi Mjini Shekhe Twahir Hussein  wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwasha moto katika jiko la gesi la Oryx wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi na majiko yake kwa viongozi wa dini pamoja na wajasiriamali wa Mkoa Kilimanjaro .Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Shaban Fundi( kulia).Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas  Shaban Fundi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoite Araman katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.

Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali mkoani Kilimanjaro wakiwa makini kupata maelezo ya umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.


Meneja Masoko wa Kampuni ya  Oryx  Gas Peter Ndomba akitoa elimu ya kutambua mtungi wa gesi ambao umepata hitilifu na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili usilete madhara kwa mtumiaji huku akieleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikihimiza matumizi salama ya majiko ya gesi.


Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...