NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali mara baada ya kufanikiwa kuinyuka 
CR Belouizdad kwa mabao 4-0 katika mchezo wa hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika.

Yanga Sc ilikuwa inahitaji ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kwani mechi ijayo ambayo Yanga Sc atacheza na Al Ahly hata kama akifungwa basi atakuwa amebaki na pointi 8 sawa na. Ambao nao wakishinda dhidi ya Medeama.

Katika mchezo huo ambao Yanga alikuwa mwenyeji na kuipa mechi hiyo PACOME DAY tumeshuhudia kandanda safi kupitia kwa Pacome na wachezaji wenzake na kufanikiwa kupata mtaji mkubwa wa mabao.

Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na Mudathir Yahya katika kipindi cha kwanza cha mchezo, mabao mengine yamefungwa na Aziz Ki, Kenned Musonda pamoja na Joseph Guede ambaye aliinhia kipindi cha pili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...