Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

KATIKA jitihada za kuunga mkono serikali kupunguza uhaba wa matundu ya choo kwa wanafunzi shuleni, Puma Energy Tanzania imefanya ukarabati mkubwa wa majengo ya madarasa pamoja na ujenzi wa matundu ya ziada ya choo pamoja na maboresho ya vifaa katika Shule ya Msingi Kisiwandui visiwani Zanzibar.

Aidha imeelezwa Shule ya msingi Kisiwandui ni ya Serikali ambayo ina wanafunzi wa kike na kiume ikiwa inapatikana Unguja, Zanzibar, ina idadi ya wanafunzi 2050 kuanzia ngazi ya awali mpaka darasa la sita, ikiwemo Watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum.

Uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa shule hiyo umefanyika leo Februari 20,2024 na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Mohamed Mussa pamoja na wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri Lela Mohamed Mussa amesema amefurahi kuona juhudi za Kampuni ya Mafuta ya Puma katika kujizatiti kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia mashuleni. “Nimefahamishwa kuwa jitihada hizi haziishii shuleni hapa Kisiwandui bali mradi utaendelea kutekelezwa katika shule tofauti visiwani Zanzibar.

“Ninawahakikishia Serikali itaendelea kushirikiana kwa ukaribu na Puma Energy, na milango yetu ipo wazi kuwasikiliza na kuwasaidia pale mtakapohitaji kutekeleza miradi ya aina hii,”amesisitiza.

Aidha imeelezwa licha ya idadi kubwa ya wanafunzi, shule ina matundu 10 pekee ya choo, idadi ambayo ni pungufu kwa viwango vya serikali ambayo inataka matundu 40 yatumike kwa wanafunzi 40. Kwa Kisiwandui, kwa uwiano wa wanafunzi 200 kwa tundu moja choo, inaonyesha uhitaji wa haraka wa kuboresha mazingira ya usafi ya shule.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdullah amehakikisha kujitolea kwa kampuni katika kuleta maendeleoc hanya kwa jamii inayoihudumia kwa kuboresha  upatikanaji wa maji safi.

Pia vifaa vya usafi wa mazingira katika shule ya msingi Kisiwandui huku akifafanua kampuni ya mafuta ya Puma imechangia Sh.milioni 130 katika mradi huo.

 “Puma Energy imeanzisha mradi wa Kuzipatia Nguvu Shule za Umma ili kuunga mkono elimu na kuhamasisha mazingira yenye afya ya kujifunzia na kuboresha matokeo bora ya elimu kwa wanafunzi wa Tanzania.

 “Wanafunzi wa Kisiwandui wanakuwa wa kwanza kunufaika na mradi huu wa Puma ambapo wamesaidiwa kuboreshewa idadi ya matundu ya choo maradufu,”amesema Fatma Abdallah.

Kuhusu Kampuni ya Mafuta ya Puma, amesema ni miongoni mwa kampuni kubwa za uuzaji wa mafuta nchini Tanzania ikitoa huduma ya usambazaji wa mafuta na vilainishi kupitia mtandao wa vituo vyake vya uuzaji wa rejareja ukihudumia jamii tofauti nchini kote.

Pia imeendelea kutanua patikanaji wa huduma kwa kujumuisha nishati ya jua na gesi na kwamba jitihada hizo ni katika kufanikisha uthibiti wa utoaji wa gesi ya ukaa na kuwaunga mkono wateja wake katika hatua hiyo.

“ Kampuni hii ni kinara katika usambazaji wa mafuta ya ndege katika viwanja vya ndege vyote nane ikiwa imewekeza takribani bilioni za Kitanzania 35 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1995 ili kuhakikisha usalama mkubwa na uendeshaji wenye viwango vya hali ya juu. “   

Pia amesema kwa Zanzibar, Puma inaendesha kituo cha kuagiza cha mafuta 2000m3 Jet-A1 na tanki la 900m3 Jet-A1 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Amesema mfumo wake wake wa kisasa wa kidigitali hupunguza ucheleweshaji na kuongeza ubora wa huduma. Puma inawapatia wateja wake - mashirika ya ndege ya ndani, kikanda na kimataifa - ambao wanahudumiwa bila ucheleweshaji.
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa( kulia) akisapeana mkono na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakati wa uzinduzi wa majengo yaliyofanyiwa ukarabati pamoja na ujenzi wa matundu ya choo katika  Shule ya Misingi Kisiwandui Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa( kulia) akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa majengo ya Shule ya Misingi Kisiwandui Zanzibar baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa sambamba na ujenzi wa matundu ya choo uliofanywa na Kampuni ya Mafuta ya Puma katika shule hiyo ambapo Sh.milioni 130 zimetumika.Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Mohamed Abdallah( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu , Maandalizi na Msingi Zanzibar Fatuma Mode  ( wa kwanza kushoto).
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa( kulia) akivuta kitambaa baada ya  kuzinduliwa kwa majengo ya Shule ya Misingi Kisiwandui Zanzibar baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa sambamba na ujenzi wa matundu ya choo uliofanywa na Kampuni ya Mafuta ya Puma katika shule hiyo ambapo Sh.milioni 130 zimetumika.Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Mohamed Abdallah( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu , Maandalizi na Msingi Zanzibar Fatuma Mode  ( wa kwanza kushoto).

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatuma Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa majengo yaliyofanyiwa ukarabati pamoja na ujenzi wa matundu ya choo uliofanywa katika Shule ya Msingi Kisiwandui Zanzibar ambapo kampuni hiyo imetumia Sh.milioni 130 katika kufanya ukarabati huo
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa pamoja na ujenzi wa matundu ya choo katika  Shule ya Msingi Kisiwandui Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa( kulia) akivuta kitambaa baada ya  kuzinduliwa kwa majengo ya Shule ya Msingi Kisiwandui Zanzibar baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa sambamba na ujenzi wa matundu ya choo uliofanywa na Kampuni ya Mafuta ya Puma katika shule hiyo ambapo Sh.milioni 130 zimetumika.Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Mohamed Abdallah( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu , Maandalizi na Msingi Zanzibar Fatuma Mode  ( wa kwanza kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...