Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma

Serikali kupitia Taasisi yake ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Nchini imefanikiwa kukamata dawa za kulevya za aina mbalimbali zenye uzito wa Kilo Gram million 1,965,340.52 kwa mwaka 2023 ikiwa ni karibia Mara tatu ya miaka 11 iliyopita.  

Taarifa hii imetolewa leo hii Jijini Dodoma na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mh Jenista Mhagama wakati akitoa taarifa hii kwa waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali katika kupambana na Kuzuia Biashara na Matumizi ya dawa za kulevya.

Na kuongeza kuwa hii inaashiria kuwa kasi imeongezwa katika mapambano ikiwemo uwepo wa mbinu za kientelensia kwa Watumishi na kutoa mafunzo mbalimbali ya uthibiti wa dawa za kulevya.

"Kuanzia January mpaka December mwaka 2023 Mamlaka imefanikiwa kukamata aina mbalimbali za dawa za kulevya zenye uzito wa Kilo Gram 1,965,340.52 katika maeneo tofauti Nchini. Na kuendana na dawa hizo zilizokamatwa  pia watuhumiwa 10522 ambao Kati ya wanaume walikuwa 9701 na wanawake ni 821 waliokamatwa wakihusianishwa na shehena hiyo ya dawa za kulevya ambazo Mamlaka ilifanikiwa kuzikamata".

"Katika hicho pia Cha January mpaka December Mamlaka ilifanikiwa kuteketeza hekari elfu 2,924 ambayo yalikuwa ni mashamba ya Bangi na Mirungi".

Aidha Waziri Mhagama ametoa ufafanuzi kuhusu kuongezeka kwa ukamataji wa dawa za kulevya katika mwaka huu Mmoja wa 2023 ambapo amesema kuwa kasi imeongezwa,lakini pia dhamira iliyo thabiti pamoja na uwepo wa vifaa vya kiteknolojia katika Mamlaka hii.

"Kuna Jambo ningependa mfahamu kwa kipindi cha miaka 11 iliyopita tulifanikiwa  kukamata shehena za dawa zipatazo Kg 606,465 tu,lakini kwa mwaka Mmoja ndo tumefika kwenye hiyo kg zaidi ya milioni moja. Lakini pia Serikali imefanikiwa Kuzuia uingizaji wa Kg 157,738.55 ya kemikali Bashirifu ambazo kama zingeingia zingeweza kutengeneza dawa za kulevya ambazo ni kinyumr na sheria na kuleta madhara".

"Pia sababu za kufanikiwa kwa hayo yote ni Serikali kuongeza kasi,Utashi wa uongozi wetu,Dhamira iliyowekwa ,uwepo wa vifaa vya kiteknolojia katika mapambano haya pia kutoa mafunzo ndani na nje ya Nchi kwa Watumishi kuhusu Interejensia  kwa ujumla ya mapambano haya dhidi ya biashara na Matumizi ya dawa za kulevya, kuongeza Watumishi na Uzalendo walionao Watumishi ndani ya Mamlaka".

Sambamba na hayo yote pia amesema Sasa Sasa imejikita katika utoaji wa elimu kuhusu mapambano haya kuanzia ngazi ya Elimu ya msingi, Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo vya Elimu ya juu.

"Serikali imejikita katika utoaji wa elimu,tumeamuamua kuelekeza nguvu zetu kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, Vyuo vya Elimu ya Kati na Vyuo vya Elimu ya juu na kuunganisha nguvu na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa PCCB  Mana wao walishaingia katika Taasisi ya Elimu na kuanzisha Clubs mbalimbali za wanafunzi za kutoa elimu juu kuoinga rushwa, hivyo Sasa club hizo zitakuwa zinatoa elimu ya kupinga rushwa na kupambana na dawa za kulevya".

Pia Waziri Mhagama ameeleza kuwa tafiti zilizofanywa na Mamlaka zinaonesha kuwa Matumizi ya dawa za kulevya yanaanza kwa watoto tangu wakiwa wadogo hivyo wameona ni vema kuwasaidia watoto hao tangu waki ngazi ya Elimu ya chini kabisa.

"Tafiti zilizofanywa na Mamlaka hivi karibuni tumegundua Matumizi haya ya dawa za kulevya yanaanza na watoto wadogo tena wakati mwingine ni kuanzia miaka 10-12 wanakuwa wameingia kwenye uraibu wa matumizi wa dawa,kwahiyo Serikalini imejidhatiti kwa kuweka mpango wa kuweza kuwalinda hawa watoto kuanzia wakiwa wadogo, maana mpango mkakati wetu unajikita kule katika shule za sekondari ambako hawa ndiko wanakoanza kujifunza.

Dhamira hii ya Mapambano dhidi ya Biashara na Matumizi ya dawa za kulevya imesimamiwa vyena na Dkt Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa mwaka 2023 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...