WACHEZAJI wa klabu za Ukanda wa pwani wanatarajia kuoneshana ufundi kwenye katika Shindano la "CRDB BANK INTER CLUBS COMPITION " Machi 9,2024 viwanja vya Lugalo gofu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 29,2024 Afisa Habari Lugalo Gofu Meja Selemani Semunyu amesema shindano Hilo linalengo la kushindanisha Klabu za Gofu zilizopo ukanda wa Pwani ili kuendeleza Umoja na mshikamano uliopo katika Klabu hizo katika Mchezo huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo Cha Wateja binafsi ya Benki ya CRDB Stephen Adili amesema Michezo ni Ajira na chanzo Cha fursa nyingi hivyo wanatarajia Wachezaji watakao shiriki Shindano Hilo wataweza kudumisha mahusiano pamoja na wateja wao wa zamani na wapya.

Hata hivyo Adili amesema benki ya CRDB itaendelea kutoa ushirikiano katika michezo hususani mchezo wa gofu kwani anaamini mchezo huo unaleta ushirikiano, mahusiano na umoja baina ya watu wanapokusanyika kufurahia mchezo huo.

"Tunaamini mchezo huu wa gofu utaenda kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kwenye vilabu hivyo na watu wengi wanaajiriwa kupitia michezo hivyo sisi kama CRDB tunaamin sekta hiyo inahitaji kupewa kipaumbele zaidi ndio maana tumeamua kuunga mkono shindano hili ."

Pia amesema kwenye mchezo wa mpira wa miguu wameendelea kufanya vizuri na kushirikiana na klabu kubwa ikiwemo Simba na yanga na malengi yao kuendelea kutoa ushirikiano katika klabu zingine pamoja na Michezo mingine ili kuonesha Benki hiyo inajali michezo yote nchini.

Hata hivyo Nahodha wa Klabu hiyo Meja Japhet Masai amesema, shindano Hilo litachezwa Kwa Mfumo wa "Match Play-Stroke Play Hole by Hole" Wachezaji wawili wa Klabu Moja watashindana na Wachezaji wawili wa Klabu nyengine.

''Shindano hilo litatoa Wachezaji wawili katika kila klabu kushindana na Wachezaji wengine hivyo nawakaribisha sana klabu hizo ziweze kushiriki shindano hilo litakalofanyika siku moja na tunategemea mchezo huo utafanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na ushirikiano tuliopewa na wadhamini wetu ."

 

Msemaji wa Klabu ya Lugalo gofu Meja Selemani Semunyu akizungumza na Wanahabari Leo Februari 29,2024 wakati akitambulisha shindano la "CRDB BANK INTER CLUBS COMPETITION " linalotarajiwa kufanyika Machi 09,2024 Viwanja vya Lugalo Gofu Jijini Dar nikushirikisha Klabu za Ukanda wa pwani ikiwemo Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana, Morogoro Gymkhana pamoja na wenyeji wa shindano Klabu ya Lugalo gofu
 

Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi kutoka Benki ya CRDB Stephen Adili akizungumza na Wanahabari Leo Februari 29,2024 kama sehemu ya wadhamini wakuu wa shindano la "CRDB BANK INTER CLUBS COMPETITION " Litakalohusisha Klabu Tatu za Ukanda wa pwani ikiwemo Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana, Morogoro Gymkhana pamoja na wenyeji wa shindano hilo Klabu ya Lugalo gofu Machi 09,2024  ambapo amehaidi benki ya CRDB itaendelea kutoa ushirikiano katika mchezo wa gofu ili kukuza mahusiano mazuri na wateja wa benki hiyo pamoja na mashabiki wa michezo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...