Kikosi cha Tabora United leo kitaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Namungo ya Ruangwa Mkoani Lindi utakaochezwa Februali 11 katika Uwanja wa Alhasan Mwinyi Mjini Tabora.

Tabora United Chini ya Kocha Mkuu Goran Copunovic wataingia kwenye mazoezi jioni ya leo ikiwa ni siku moja tangu ilipotoka kupoteza mchezo wake dhidi ya Simba Februali 06 mwaka huu kwa magoli manne kwa bila.

Tabora United baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Simba Kocha Goran alitoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji na kwamba leo hii Timu inaingia tena kwenye uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kujiweka vizuri ili kumaliza mzunguko wa kwanza siku ya Jumapili.

­” Tumetoka kupoteza mchezo muhimu na Simba tukiwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani matokeo ambayo yalimuumiza kila mmoja wetu, lakini tayari tumeshamaliza mchezo huo kikubwa kama Timu tunaangalia nafasi nyingine ambayo tunayo kwa Namungo.

Tunajua kabisa huu mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na kwamba Namungo wanatimu nzuri, benchi zuri la ufundi lakini tunakwenda kwenye uwanja wa mazoezi kujiandaa ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi makosa ambayo yalijitokeza kwenye mchezo uliopita lakini pia ikumbukwe kwamba Timu bora sikuzote haipotezi mchezo mara mbili.

Hata hivyo kwa upande wa Afya za wachezaji wote wapo vizuri na kwamba kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo unaokuja na kwamba mashabiki na Watanzania wote tunawaomba waendelee kutuunga mkono kwenye michezo yetu ya nyumbani na ile ya ugenini kwa lengo la kufanya vizuri.

Tabora United ipo kwenye nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC soka Tanzania bara ikiwa na jumla ya alama 15 na imecheza michezo 14 hivyo tunaendelea kuwasihi mashabiki zetu wasiwe na hofu na msimamo huo kwakuwa tunaamini tutatoka na kupanda kwenye nafasi za juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...