Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma

Serikali ya Tanzania ipo kwenye maandalizi ya uchumi wa kidijitali kutoka mwaka 2024 hadi mwaka 2034 utakaowezesha mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya fedha tathimini ndani ya jamii.

Mohamed Abdi mashaka ni Mkurugenzi wa uendelezaji wa mifumo huduma za TEHAMA ameyabainisha hayo jijini Dodoma katika kikao kazi cha wakurugenzi na wakuu wa TEHAMA kutoka Wizara ya Habari, Mnawasiliana na Teknolojia ya habari.

Mkurugenzi huyo amesema mkakati huo wa kidijitali una nguzo sita

" Kupeleka mtandao Vijijini hata wakulima nao waweze kuuza mazao yao kimtandao na huo ndiyo uchumi wa kidijitali tunaouzungumzia.

Amesema mkakati huo umegusa maeneo mbalimbali na kuona ni kwa jinsi gani jamii itaweza kupunguza fedha toka mikononi na kuweza kutumia fedha hizo kwa njia ya TEHAMA.

Naye David mwankenja ,Mkurugenzi wa sera na mipango kutoka wizara ya habari ,mawasilano na Teknolojia ya habari amesema lengo ni kukusanya kwa pamoja jitihada zote za TEHAMA ndani ya Serikali ili kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha kuwa jitihada hizo zinaleta matokeo yaliyotarajiwa na ni Mpango wa miaka 10 kuanzia mwaka huu 2024 mpaka mwaka 2034 na katika kipindi hicho itaonekana ni jinsi gani TEHAMA itakavyoweza kusaidia Kimataifa Kupita uchumi wa kidijitali.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...