Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amezindua mradi wa kusaidia kaya 482 zilizoathiriwa na Mvua kubwa iliyonyesha Mwaka jana ikiamabatana na upepo mkali na kusababisha maafa makubwa kwa baadhi ya Kaya katika Wilaya za Muleba na Bukoba Manispaa.

Katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Hotel, mapema Februari 19, 2024 kupitia Shirika la Tanzania Christian Refugees Service (TCRS) chini ya Kanisa la Kiinjili la kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesisitiza juu ya Wale wanaotakiwa kunufaika na Mradi huo ni wale walengwa ambao tayari tathimini ilishafanyika kwao na kutambuliwa.

‘..Matarajio ya mradi huu ni kusaidia Kaya 482, Ambapo wanakaya wa kaya hizo watahudumiwa mahitaji ya chakula, uboreshaji makazi, msaada wa kisaikolojia, maji safi na usafi wa mazingira, elimu juu ya usalama wa chakula na kuwajengea uwezo wa kiuchumi kujiongezea kipato, nasisitiza Fedha zitakazotolewa kwa kaya zitumike kwa matumizi yaliyolengwa na kisiwe chanzo cha Ndoa kuvunjika na kusababisha ukatili wa kijinsia katika familia…’ Amesema Mhe. Mwassa.

Itakumbukwa kuwa Tarehe 15 Oktoba 2023 ilinyesha Mvua kubwa na kusababisha maafa Wilaya ya Kata za Karambi na Kasharunga, ambapo nyumba za Wananchi 221, Shule 4 ziliezuliwa, mashamba yenye ekari 125 yaliharibiwa Pamoja na miundo mbinu ya Umeme, huku kwa Manispaa ya Bukoba Kata za Kashai, Rwamishenye, Bilele na Hamugembe pia yakitokea maafa kama hayo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...