VIONGOZI ya dini ya Kiislamu pamoja na waumini wa dini hiyo na wananchi kwa ujumla leo wameingia katika siku ya pili ya kuendelea na dua maalum ya kuliombea Taifa pamoja na viongozi wote.


Katka dua ya leo Ijumaa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Bin Zubeir akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini pamoja na Mjumbe wa Halmashauri  ya BAKWATA Ahmed Misanga ni miongoni walioshiriki katika dua hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba imeelezwa kuwa leo Ijumaa ni siku ya pili ya mwendelezo wa wa dua hiyo kubwa iliyotangazwa kufanya na Mufti wa Tanzania kwa mfululizo wa siku tatu na kilele cha dua hiyo ni Februari  24 mwaka huu ambayo itakuwa Jumamosi.

Kilele cha dua hiyo  katika viwanja vya Msikiti wa Mfalme Mohammed VI BAKWATA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam huku ikisisitizwa katika siku hiyo dua itaanza saa mbili asubuhi hadi saa 10 alasiri.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...