NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Songea

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani amewahimiza waajiri nchini kujisajili na kutoa taarifa za ajira za wafanyakazi wao kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili kulinda haki za wafanyakazi hao pindi wanapopatwa na majanga wakiwa kazini.

Mhe. Jaji Siyani ameyasema hayo mjini Songea wakati akifungua Kikao Kazi cha Mafunzo kuhusu sheria ya fidia kwa wafanyakazi kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kusini, watendaji wa mahakama na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

"Pamoja na uwepo wa sheria inayowabana waajiri wanaoshindwa kuwasajili wafanyakazi wao WCF lakini bado kuna waajiri ambao hawatoi taarifa za ajira za wafanyakazi wao na hivyo kuuweka mfuko katika nafasi ngumu ya kutekeleza majukumu yake," amefafanua.

Jaji Siyani ametoa mfano wa kisa cha mfanyakazi mmoja aliyekuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja ya ujenzi mkoani Lindi ambaye aliumia akiwa kazini na kupelekea kupoteza  baadhi ya viungo vyake na kumsababishia ulemavu wa kudumu kwa zaidi ya asilimia 75 lakini alikosa vigezo vya kupata fidia kwa kuwa mwajiri wake hakuwa amejisajili na kuwasilisha michango WCF kwa mujibu wa sheria.

“Licha ya kijana huyo kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili lakini taarifa zake hazikuwepo WCF na hivyo kukosa haki ya kupata fidia yoyote” ameeleza Jaji Siyani; na kuongeza kuwa iwapo zingekuwepo taarifa za mfanyakazi huyo, bila shaka angepata fidia bora zaidi ya ile iliyotokana na majadiliano na maridhiano na mwajiri wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, amesema Mahakama ya Tanzania ni wadau muhimu wa Mfuko huo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kuwa Mfuko unategemea maamuzi mbalimbali ya mahakama katika utekelezaji wake wa majukumu ikiwemo maamuzi ya kesi za mirathi.

Dkt. Mduma amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali  yanayozitaka  taasisi zake kuhakikisha zinashirikiana kwa karibu kwa dhumuni la kuongeza tija na huduma bora kwa wananchi.

Pia, mafunzo hayo yanatoa fursa ya kubadilishana uzoefu baina ya wataalam wa Mahakama na WCF kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa ambapo washiriki wanaweza kuja na mapendekezo yatakayoboresha utendaji kazi wa Mfuko huo.

"Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya yataleta manufaa makubwa kwa pande zote mbili, ikiwemo kuimarisha mahusiano kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi na kuchangia kukuza uchumi wa nchi yetu na hasa kupunguza umasikini kwa wafanyakazi watakaopata majanga yanayotokana na kazi zao," amesisitiza Dkt. Mduma.

Mafunzo hayo ambayo ni ya awamu ya nne yamewaleta pamoja washiriki kutoka mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Iringa, Mbeya, Songwe na Rukwa ambapo miongoni mwa mada zinazotarajiwa kuwasilishwa ni kuhusu sheria ya fidia kwa wafanyakazi, taratibu za uwasilishaji na ushughulikiaji wa madai ya fidia kwa wafanyakazi.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohammed Siyani, akizungumza kwenye kikao kazi cha Mafunzo ya Uelimishaji kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kusini na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), mjini Songea, Februari 9, 2024.

JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohammed Siyani (katikati), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia) na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha, akizungumza kwenye kikao kazi cha Mafunzo ya Uelimishaji kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kusini na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), mjini Songea, Februari 9, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (aliyesimama kushoto), akizunguzma na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kusini na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Songea, Februari 9, 2024. Pamoja nae kutoka kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohammed Siyani, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina.

Baadhi ya washiriki

Baadhi ya washiriki

Baadhi ya washiriki

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohammed Siyani (kushoto), akikabidhiwa vitendea kazi vya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohammed Siyani (katikati) akipeana mikono na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (kushoto) huku Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia) na Jaji Mfawidhi Mahakama KUU Knada ya Songea, Mhe. Mhe. James Karayemaha wakishihudia 

Meza Kuu katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Meza Kuu katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi.
Meza Kuu na watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)
Meza Kuu katika picha ya pamoja na wanufaika wa fidia kutoka WCF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...