Na Jane Edward, Arusha 

Muarobaini wa changamoto ya upatikanaji wa umeme nchi umeanza kupata ufumbuzi baada ya wadau wa sekta ya nishati ya umeme kukutana jijini Arusha kujadili njia mbadala za upatikanaji wa umeme katika nchi hizo.

Hayo yamebainishwa na kamishna wa nishati jadidifu kutoka wizara ya nishati mhandisi Innocent Luoga katika mkutano uliowakutanisha mawaziri kutoka nchi tano za Afrika ikiwemo Malawi, Ethiopia na Uganda lengo likiwa ni kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya nishati na kubadilishana uzoefu.

Aidha amesema  katika mkutano huo azimio kubwa linaloenda kufanyika ni kutumia vyanzo mbadala vya upatikanaji wa umeme ikiwemo matumizi ya upepo, joto ardhi, nishati ya jua, maji na gesi.

"Katika kutatua changamoto ya umeme sisi Tanzania tayari tuna miradi mikubwa ya kuunganisha umeme nchi jirani na sasa tunaunganisha umeme Tanzania na Kenya ambapo utatokea Singida, Arusha, unapitia namanga mpaka Isinya nchini Kenya" Alisema.

 Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupambana na suala la mdororo wa kiuchumi unaosababishwa na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara jambo linalopelekea wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao. 

Kwa upande wake mtendaji Mkuu wa shirika la umeme Tanzania TANESCO hapa nchini ,Gissima Nyamo-Hanga amesema amekuja katika mkutano huo kimkakati na kuangalia mashirikiano ya wadau mbalimbali wa nishati na kuleta mawazo ya kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika.aa

Ameongeza kuwa katika kipindi cha hivi karibuni wamejipanga kama shirika kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia umeme wa joto ardhi.

Akitoa wito kwa watanzania mkurugenzi amesema suala la umeme wa uhakika lipo mbioni kukamilika na watanzania watapata umeme wa uhakika hivyo amewataka kuwa walinzi wa miundombinu ya TANESCO .

Mhandisi Innocent Luoga kamishna wa nishati jadidifu kutoka wizara ya nishati nchini akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Mtendaji Mkuu wa shirika la umeme Tanesco Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Arusha.

Washiriki wa Mkutano wakiendelea kufatilia mijadala kuhusu nishati ya umeme.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...