Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya Uhasibu.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Shirika CPA Kulwa Malendeja amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kuwa Mhasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Aliongeza kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi alisema Malendeja.

Naye Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA. Bertha Kipangula ametoa elimu kuhusu tofauti iliyopo kati ya Mkaguzi na Mhasibu na kuainisha kazi za wakaguzi kwa wanafunzi wa Kidato cha tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea ofisi za Bodi ya NBAA Dar es Salaam ili kujifunza juu ya Taaluma hiyo.

Akiishukuru Bodi hiyo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi amesema Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imetoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa wanaosoma masomo ya biashara katika shule hiyo na elimu hiyo iliyotolewa itawasaidia wanafunzi wa Baobab katika masomo yao na kwa hapo baadae.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Shirika CPA Kulwa Malendeja akizungumza kuwakaribisha pamoja na kufungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Utumishi NBAA, Gloria Kaaya akitoa historia ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) tangu kuanzishwa kwake wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo akitoa elimu ya namna na kujiunga na masomo ya Bodi kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Mhasibu kutoka NBAA, CPA Yusuph Lema akiwasilisha mada kuhusu utengenezaji wa Taarifa za Kifedha  kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA. Bertha Kipangula akitoa elimu kuhusu kazi za wakaguzi kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBA.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab wakifuatilia mada kwa wataalam kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi akitoa neno la shukrani kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) mara baada ya wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab mara baada ya kumaliza ziara yao walipotembelea ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya Wafanyakazi wa NBAA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab mara baada yakumaliza ziara ya kutembelea ofisi za NBAA zilizopo jijii Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiwatembeza wanafunzi kwenye maeneo mbalimbali ya Bodi ya NBAA wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...