NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WADAU wa Jinsia na Maendeleo (GDSS) wameishauri Serikali kutunga sheria ambayo itatoa adhabu kwa watakaobainika kufanya vitendo vya ukeketaji kwenye jamii,ambapo mtoto wa kike na mwanamke atakuwa amekombolewa katika ukatili huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2024 Mwanaharakati wa Jinsia Bw.Nobart Dotto amesema serikali itunge Sheria ambayo itasimamiwa na wao kuwasaidia kuibua watu wanaofanya hivyo vitendo waweze kuwajibika kulingana na Sheria


Aidha amesema kuwa wamekubariana kutengeneza mabango yenye ujumbe yasambazwe katika jamii kwa lengo la kukomesha kabisa suala hilo la ukeketaji pamoja na kutumia maafisa ustawi ambao wataijulisha serikali pale tu kunapotokea jambo hilo na kuwahudumia wahanga.


Kwa Upande wake Mwana GDSS kutoka taasisi ya Young and Alive Intiantive Bi.Esther Mshana amesema katika mafunzo hayo wamepewa ujuzi wa kutambua endapo ukatili huo umepangwa kufanyika katika eneo hilo.


"Tumefundishwa tutumie viashiria Kutambua ngariba wanatumia nini wengine walisema unaweza kukuta anatumia kipisi Cha kanga hapo ndipo utatambua kuwa kunashughuli"Bi.Esther amesema


Amesema wameadhimia kuwa na kitini kwa ajili ya kuwa na nyenzo ya kufundishia watu katika Jamii inayowazunguka kupitia nguvu za Pamoja kukea suala hilo la ukatili.


Aidha Bi.Esther amesema kuwa amejitoa kutoa taarifa kwa serikali ya mtaa kupinga ukatili huo kwa Wasichana na wanawake ambapo itasaidia kuondoa kabisa ukeketaji katika eneo lake.


Pamoja na hayo ameeleza kuwa sababu inayopelekea wakubali kuketwa ni uwepo wa mila potofu katika baadhi ya makabila ambayo inamshurutisha binti akubali kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...