*TCRA yaahidi kutoa elimu zaidi ya mawasiliano

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za wizi wa mitandao ili kuwadhibiti wizi hao lakini pia kutumia mitandao kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

Hali ya utumiaji wa mawasiliano umeinarika nchini kwa wanaotumia simu janja ni milioni 19.8 na laini za simu zilizosajiliwa milioni 70

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam februari 2,2024 na Mkurugenzi Mkuu TCRA, Dkt. Jabir Bakari wakati akifungua semina ya kwa ajili ya kuelimisha wadau wa masuala ya mtandao wa intaneti katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya usalama mtandaoni .

Amesema kila mtumiaji wa mawasiliano kuhakkisha anga iko salama na watumiaji kuwa salama katika kutumia mawasiliano hayo.

Dkt. Jabir amesema ni muhimu elimu kuhusu usalama wa mtandao kutolewa kwa kila nyanja ili kudhibiti wahalifu hao na pengine kuwatoa katika kundi hilo na kuingia kwenye kuelimisha usalama wa mtandao.

Amesema kuwa baadhi ya watumiaji wanatumia mitandao kwa kufanya uhalifu ambapo jambo hilo TCRA inaendelea kutoa elimu.

"kuna haja ya kuwadhibiti wanaotumia mitandao vibaya kwa kufanya matukio ya utapeli kuiba taarifa binafsi za watumiaji wengine kwa lengo la kujinufaisha wenye na hata kuleta matatizo Kwa wengine"Amesema.

Amesema pamoja na faida za mitandao bado ipo haja kwa wahalifu wa mtandao kudhibitiwa na kupewa elimu ili waweze kutoka kwenye kundi hilo la uhalifu na kuwaelimisha wengine kuhusu usalama wa mitandao.

"Pamoja na faida nyingi zitokanazo na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano bado tunaowajibu wa kuendelea kuelimishana kwani kuna baadhi ya watumiaji wanatumia fursa ya Tehama na nyingine zinazoletwa na Tehama vibaya Kwa kufanya uhalifu hivyo tunawajibu wa kuwadhibiti "alisema na kuongeza kuwa

"Kupitia mitandao unaweza kuongeza kipato na pengine kuwa na ubunifu ama ajira jambo linaloweza kubadilisha maisha ," amesema Bakari na kuongeza kuwa teknolojia ya kidigiti inaongezeka wigo wa Mawasiliano.

Ametolea mfano kuwa dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda anayetumia Tehama anafikiwa na fursa nyingi kuliko asiyekuwa na nafasi hiyo.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya robo ya mwaka ya Desemba mwaka 2023 imeonesha kuwa watumiaji wa intaneti katika nchi ya Tanzania wamefikia takribani 35.8 huku idadi za simu janja ambazo zinauwezo kutumia intaneti ni millioni 19.8.

"Dhana za maendeleo ya teknolojia ya kidigiti kila mmoja ananafasi muhimu ya kuhakikisha angala la mtandao ni salama kwa kuzingatia matumizi sahihi na salama na kuleta tija kwa kila mtu, binafsi pamoja jamii"amesema Dkt Bakari

Kwa upande wake mmoja wa washiriki katika semina hiyo Dkt Macca Abdalla ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya madirisha women cooperative sector amesema kuna haja ya kuendelea kuelimisha wanawake matumizi ya mtandao katika kufanya biashara zao kwani wengi wamekuwa wakidhurumiwa na wengine kufanya udanganyifu katika bidhaa wanazoziuza.
Mkurugenzi Mkuu TCRA, Dkt. Jabir Bakari wakati akizungumza wakati  akifungua semina ya kwa ajili ya kuelimisha  wadau wa masuala ya mtandao wa intaneti katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya usalama mtandaoni jijini Dar es Salaam.
 

Mkurugenzi wa Idara ya Leseni wa TCRA  John Daffa akitoa maelezo kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Watumiaji wa Internet ,jijini Dar es Salaam.
 

Baadhi ya washiriki wa Semina iliyoratibu semina ya wadau wa mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...