Na Jane Edward, Arusha

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda,amehitimisha siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake na wasichana katika Sayansi mkoani Arusha huku akisisitiza kuwekeza katika sayansi kwa kuwapatia vijana fursa ya ajira.

Akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo kauli mbiu ni "Wanawake na wasichana katika uongozi wa Sayansi Enzi mpya ya maendeleo Endelevu",Profesa Mkenda amesema ilikuendana na kasi ya Teknolojia wazazi wajikite katika kuwawekea mazingira rafiki watoto wa kike ambao yatawajenga katika kupenda masomo hayo.

Mkenda amesema wanawake na wasichana ni watu muhimu kwa mustakabali wa Sayansi iliyobora ambayo hupelekea upatikanaji wa ajira ya uhakika kutokana na kubuni vitu mbalimbali vitakavyosaiidia nchi katika maswala ya ubunifu.

"Tunapoteza sanaa kama nchi kutowapa nafasi wasichana wengine kwenda kusoma masomo ya sayansi unaweza kuwa mjasiriamali lakini bila sayansi na teknolojia hatuwezi kufika mbali tunatakiwa kuwekeza katika elimu ya sayansi na teknolojia kwasababu wenzetu wamejiwekeza katika elimu hiyo."alisema

Hata hivyo amesema Fursa za kazi duniani huko tunako enda zinategemea elimu ya TEHAMA tusipoweza kuwafundisha vijana wetu katika eneo la sayansi tunawanyima fursa za ajira " Wizara ya elimu imejipanga vizuri kuendelea kutekeleza ufadhili kwa wahitaji wotee na sisi wote na wadau wa elimu tutakuza sayansi hapa nchini natutafanya kila liwezekanalo wasichana wengi kusoma masomo ya sayansi ilikukuza uchumi wetu".alisema

"Tunatoa tuzo ya fedha kwa watafiti kati maeneo ya sayansi(utafiti) ukifanya kazi yako ukaweka katika sehemu kubwa zinazofahamika unapewa milioni 50
Nngependa nione hawa watu wanasoma sayansi zaidi Rais Samia amewekeza zaidi kwenye ujenzi wa shule za sayansi na mabweni iliwapate elimu nzuri"alisema

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Elimu Prof. Juma Hatibu kutoka chuo Cha sayansi Arusha amesema ni muhimu Kuhusisha elimu ya ubunifu na ajira ili kuweza kuwapa vijana wa kitanzania fursa katika miradi mbalimbali itakayofanywa nchini .

Elimu Bora ni elimu ya ububifu na ajira ambayo itasaidia kuondoa changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa ajira Tanzania.

"Inasikitisha sana mwaka huu tunasherehekea miaka 51 tangu kuanzishwa kwa mechanical engineering na hatuna mainjia wakujenga nchi tunaiomba serikali kupitisha sheria inayosema miradi yote ya miundombinu katika ngazi ya mkoa isipitie nje ya nchi kwasababu ili kutoa hamasa yakujifunza sayansi na teknolojia ni lazima tuunganishe na ajira kwa vijana wote wanaohitimu masomo hayo ya sayansi."alisema Profesa Hatibu

Ameongeza kuwa Katika maendeleo endelevu eneo nyeti la sayansi umma unatakiwa kujua kufanya mjadala wa masomo ya sayansi kwa watoto wa kike kwa kushirikishwa shughuli zote katika vyuo na shule za msingi na Sekondari huku walimu wa watoto hao wanaweze kufundisha kwa kutumia mbinu shirikishi.

Maadhimisho hayo yanalenga kutambua mchango wa wanawake na wasichana katika Sekta hiyo na mafanikio ya Teknolojia, uhandisi na Hisabati (STEM ).

Waziri wa elimu Profesa Adolph Mkenda akielezewa jambo na mwanafunzi wa kike kuhusu masomo ya Sayansi.


Pichani ni wanafunzi na wanawake wakiwa katika maandamano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...