Na Mwandishi Wetu Ruvuma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jensita Mhagama (Mb) Peramiho, amewapongeza wenyeviti wa mashina na Kata kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda na kukipigania Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ameitoa Wakati alipokutana na kufanya vikao na Wenyeviti wa Mashina wa Kata ya Muhukuru Lilahi, Mpitimbi Ndongosi Litapwasi katika ziara yake aliyoifanya leo tarehe 26/02/2024 Jimboni Peramiho Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Amesema Wenyeviti wa Mashina ndio wanaobeba na kusimamia ajenda ya Chama Cha Mapinduzi, na Viongozi hatutawaangusha katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

"Tunapojiandaa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, hatuna mashaka kwa sababu Viongozi wa mashina wameshaamua Jimbo hili la Peramiho ni la Chama Cha Mapinduzi," alisema.

Wanafanya hivi kumshukuru Dkt, Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa za ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika sekta ya Afya, Barabara, Nishati, Elimu na Utoaji wa Pembejeo.

Tunakila sababu ya kujivunia mambo mazuri yaliyofanywa na serikali, ili kuimarisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa Chama wa Taifa Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan anawajali nasi hatuna budi kuwajali na kuwaheshimu Wenyeviti wa Mashina.

"Tuendelee kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi, tuendelee kuwa na Imani na Mhe. Rais, tuendelee kuwa na Imani na Waheshimiwa Madiwani wetu ili mambo yetu yafanikiwe lazima tuanze mwaka huu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa" alibainisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini Ndg. Thomas Masolwa amemshukuru Mhe. Jenista Mhagama kwa kuwathamini kutembelea Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi ya Shina.

Amesema Mabalozi ni watu muhimu kwa uhai na utendaji wa kazi wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndio wanaopokea kero za wananchi.

"Niwaombe Mabalozi muendele kufanya kazi ya kusajili wanachama wapya Ile wale wasio wanachama wawe wanachama wa Chama Cha Mapinduzi," alisema

Ameongea kusema katika kujenga Chama Mabalozi wahamasishe wanachama katika kulipa Ada ya chama na kufanya mikutano na wananchi kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.


Awali Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Juma Nambaila amemshukuru nakupongeza Mhe. Jenista Mhagama kwa kutelekeza Maelekezo ya chama kivitendo kwa kupitia Ofisi za Chama.
Chama Cha Mapinduzi kimeratibiu vizuri ziara yako ya kutembelea wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi wa Shina Katika Jimbo la Peramiho wilaya ya Songea Vijijini.

"Wenyeviti wa Chama wako tayari kupokea na kutekeleza maelekezo ya serikali pamoja na maelekezo ya chama, " alibainisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...