Benki ya Letshego Faidika imetumia jumla ya sh1 billion kuwakopesha wafanyakazi wa serikali ikiwa katika mpango wake wa kuwawezesha kuwainua kiuchumi.

Hayo yalisema na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw Baraka Munisi wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la benki hiyo katika mkoa wa Kilimanjaro.

Bw Munisi alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika baada ya kufanikiwa kuwakopesha wafanyakazi zaidi 1,000 mikopo ya aina mbalimbali yenye masharti nafuu.

Alisema kuwa benki ya Letshego Faidika iliundwa mwaka jana taasisi ya kifedha ya Faidika Microfinance pamoja na benki ya Letshego Tanzania na kwa sasa wanafurahia muunganiko huo ambao umewafanya kupata mafanikio.

Alisema kuwa benki hiyo ambaypo makao makuu yake yapo nchiniBotswana, kwa sasa inafanya kazi zake katika nchi 11 tofauti na Tanzania.

“Tumeamua kufungua tawi mkoani Kilimanjaro ikiwa moja ya mikakati yetu ya kuendelea kuwasogezea huduma za kisasa za kibenki (kidigitali) Tanzania na vile vile kutoa ajira. Ni matarajio yetu kuwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watafaidika na huduma zetu kama ilivyo katika mikoa mingine na nchi nyingine 11 barani Afrika ambapo tunatoa huduma za kibeki.

Makao Makuu ya benki ya Letshego Faidika yapo nchini Botswana na pia tuna matawi Kenya, Uganda, Uganda nan chi nyinginezo,” alisema Bw Munisi.

Kwa Tanzania tupo kwenye kila mikoa na baadhi ya wilaya kwa ujumla tuna branchi na ofisi zaidi ya 110 nchini, mbali ya kuwakopesha wafanyakazi wa serikali (taasisi za umma), pia tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa makampuni binafsi, mikopo ya biashara, mikopo ya makazi n.k na vile vile huduma zingine za kibenki na utoaji wa huduma za kibima katika mikoa yote Tanzania.

Alisema kuwa mbali ya tawi hilo la kisasa, benki hiyo pia imeboresha ofisi zake nyingine maeneo ya Mwanga, Same, Rombo na Hai kwa lengo la kuwafikia wateja wao kiurahisi zaidi.

“Benki yetu inatambua umuhimu wa sekta hii ya fedha katika maendeleo ya jamii na ndio maana tumejikita katika kusogeza huduma karibu zaidi na jamii ili kurahisisha upatikanaji wake na pia kuwapa fursa wanajamii wa nyanja mbalimbali kuweza kufaidika na huduma zetu.

Hatua hii ya kufungua tawi la Letshego mjini Moshi ni ili kuongeza wigo wa kutoa mikopo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati,” alisema.

Alisema kuwa wanajivunia kuwa sehemu ya jamii ya Moshi na wamejizatiti kuhakikisha kuwa wanachangia katika maendeleo ya eneo hili na hasa kupitia ushirikiano wao na serikali na taasisi nyingine za kiserikali wenye lengo la kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wao.

“Tunawahikishia wateja wetu kuwa benki ya Letshego Faidika, itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa inaleta ubunifu, uaminifu na kujitolea katika kuhudumia jamii yetu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Br Nurdin Babua aliipongeza hatua ya benki hiyo kufungua tawi la kisasa na kuwa miongoni mwa taasisi ya kifedha zenye kutoka huduma bora mkoani hapo.

Babu ambaye aliwakilishwana Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi, Bw Shaaban Mchomvu, alisema kuwa Benki ya Letshego Faidika inakuwa kitovu cha wajasiriamali, wakulima,wafanyabiashara wakubwa na wananchi wengine.

“Nawaomba wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kutumia fursa ya benki ya Letshego Faidika katika kuboresha maisha kama ilivyo kauli mbiu yako,” alisema Bw Mchomvu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...