Wizara zetu hizi mbili kwa kuendelea kuimarisha mahusiano haya na yanatusaidia kwa kiasi kikubwa’’ alisema Bw. Uweje.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bonanza la Pasaka ambaye pia ni Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mgusi Musifa, alisema kwa mwaka huu Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo imefanya maboresho katika Bonanza ikilinganishwa na miaka ya nyuma hususani katika mchezo wa mpira wa miguu kutokana na kuweka timu mbalimbali za nje mbali na timu ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.

"Tukiongelea histori ya nyuma wakati huu tumeboresha kidogo, kwa sababu kawaida tulikuwa tukicheza sisi Hazina Bara na Hazina visiwani lakini leo tumekuwa na timu sita’’ aliongeza Bw. musifa.

Tamasha hili la Pasaka limekuwa likifanyika kwa zaidi ya miaka ishirini sasa na limekuwa likifanyika kwa kuunganisha pande zote mbili za Muungano kwa miaka yote hiyo. Na timu zilizoshiriki ni pamoja na timu ya Maveterani kutoka Bara na visiwani,Police FC, Hazina Sports club, GPSA, PSPTB, Area C na nyingine zao
 

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (wapili kulia), akizungumza katika Bonanza la Pasaka lililofanyika katika viwanja vya Kilimani Jijini Dodoma, lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake, Bonanza hilo linaambatana na matendo ya huruma yatakayofanyika tarehe 31/03/2024.
 

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, akikagua timu za mpira wa miguu zikihusisha wachezaji kutoka Wizara ya Fedha-Bara na wachezaji kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, kabla ya kuanza kwa mchezo huo katika uwanja wa Kilimani Jijini Dodoma, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha-Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake.
 

Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumza, kwa niaba ya Mkurugenzi, Utumishi na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Suleiman Mohammed Rashid, wakati wa kufungua Bonanza la Pasaka kwa niaba ya Mkurugenzi wa Utumishi, na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Suleiman Mohamed Rashid, lililofanyika katika viwanja vya Kilimani Jijini Dodoma, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha Tanzania Bara, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake
 

Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumza, na Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mgusi Musifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bonanza la Pasaka, mara baada ya mapumziko mafupi ya mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika katika Uwanja wa Kilimani kati ya Wizara ya Fedha-Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, katika mchezo huo timu hizo zimetoka suluhu.
 

Picha za matukio mbalimbali ya watumishi kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, wakishiriki michezo ya kuvuta kamba na mpira wa miguu kwa wanaume, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha Tanzania Bara, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, pamoja na Taasisi zake, michezo hiyo imefanyika katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...