Raisa Said,Bumbuli

Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imetangaza mikakati kadhaa yeye lengo la kuinua kiwango cha ufaulu na elimu kwa ujumla katika halmashauri hiyo.

Kwa muijibu wa Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Baraka Ziakatimu, Halmashauri imelenga kuongeza kiwango cha ufaulu wa mtihani wa upimaji kidato cha pili kutoka asilimia 84 hadi kufikia 100 na wa kidato cha nne kuongezeka kutoka asilimia 89.58 hadi kufikia 95.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmshauri hiyo, aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja kutoa motisha ya fedha taslimu kwa wanafunzi, walimu na shule zitakazofanya vizuri.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wamepanga kutoa motisha ya Sh million 3 kwa kila shule ya sekondari ambayo itakuwa na ufaulu wa divisheni 1 kwa wanafunzi wote (asilimia 100). Kuna jumla ya shule 29 za sekondari za kata katika Halmashauri hiyo.

Alieleza kuwa shule ambayp itakuwa na divisheni ya pili itapata Sh milioni 2 wakati shule ambayo itakuwa haina divisheni zero Wala four itapata Sh milioni moja.

Kwa upande wa walimu, Zikatimu alisema kuwa wanafunzi 10 wakipata daraja la A katika somo husika mwalimu atapata shs 10,000 na zikiongezeka anapata sh 2000 kwa kila mwanafunzi aliyepata A.

Pia alieleza kuwa mwalimu atakuwa anapata Sh 5,000 kama wanafunzi 20 watapata daraja la B na wataongezwa sh 2,000 kwa kila mwanafunzi anayeongezeka na zikifika 41 atapata shs 3000 kwa kila mwanafunzi.

Akizungumzia kuhusu mwaka huu, alisema kuwa shule zote 29 za sekondari zitapatiwa mitungi ya jiko la gesi kwa ajili ya walimu kupikia chakula chao cha mchana kwenye maeneo ya shule.

Halmashauri hiyo mwaka huu imetoa jumla ya Sh milioni 3.63 kama motisha kwa walimu 134 waliowawezesha wanafunzi kupata ufaulu wa Daraja A na B katika mitihani ya upimaji wa kidato cha pili.

Pia Halmashuri imetoa motisha ya jumla ya Sh millioni 4.11 kwa walimu 118 waliowawezesha wanafunzi kupata ufaulu wa daraja A na B katika mitihani ya kidato cha nne. Pia imetoa motisha ya jumla ya Sh 300,000 kwa walimu watatu wa taaluma kutoka shule za serikali zilizofuta daraja sifuri katika mitihani ya kidato cha nne. Shule hizo ni Mgwashi, Kizanda na Kizimba.

Naye Afisa Elimu Elimu Taaluma (Sekondari), Simon Shelukindo, alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili elimu kuwa ni pamoja na walimu kukaa kwenye vituo kwa muda mrefu hali inayowafanya kufanya kazi kwa mazoea. Alisema hali hiyo inasabishwa na ukomo wa bajeti ya Msawazo kwa walimu (Uhamisho) kuwa finyu.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni wanafunzi wanaofeli kidato cha pili kutorejea shule wakati ambapo serikali imetoa nafasi ya a hawa kurudia shule pindi alama za ufaulu kutokidhi kuendelea na kidato cha tatu.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni walimu kutopandishwa madaraja kwa wakati uchangiaji hafifu wa chakula cha mchana shuleni kwa baadhi ya wazazi au walezi na matumizi duni ya lugha ya kiingereza kwa walimu na wanafunzi hali inayosababisha wanafunzi kutopata maarifa na ujuzi uliokusudiwa mwanafunzi kuumudu kwa ngazi ya elimu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Amiri Shehiza alitaja baadhi ya changamoto ambazo alisema zinakabili utekelezaji wa shughuli za elimu kuwa ni pamoja wanafunzi kutembea umbali mrefu kwa baadhi ya maeneo kuzifikia shule wanazopangiwa huku wanafunzi wengine wakitembea zaidi ya kilometa tatu kuika shuleni kwa baadhi ya maeneo,

Pia alitaja changamoto ya upungufu wa miundombinu muhimu ya shule hususan katika shule za sekondari. Miundombinu hiyo ni pamoja maabara za sayanzi, vyumba vya madarasana nyumba za walimu.

Hata hivyo, alisema kkatika mwmaka 2022/23 serikli inaoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya Sh Bilioni 1.16 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu ikiwemo ujenzi wa nyumba nane za nane walimu katika shule nne ambazo hazikuwa na nyumba za walimu (Sh milioni 228 kutoka tozo ya mawasiliano.

Miradi mingine ni ujenzi wa shule ya sekondari ya Kwehangala kupitia mradi wa SEQUIP (Sh mlioni 584,) ukamilishaji wa maboma ya maabara za sayansi katika shule tatu (Sh milioni 150) na ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule saba (Sh milioni 200).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...