Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Katika kurudisha kwa jamii, kampuni ya Insignia Limited imetoa msaada wa ndoo za rangi kwa ajili ya ukarabati wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili ( MOI) wenye thamani ya shilingi milioni 10 za Kitanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili ( MOI ) Profesa Abel Makubi amepokea msaada huo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuisaidia taasisi hiyo kwa sababu ina mahitaji makubwa.

" Tunahudumia kundi kubwa la wananchi kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini,"

" Tuna watu wanaopata ajali mbalimbali wakiwemo wenzetu wa bodaboda na watu wengine wanakuja hapa kupata matibabu ni maskini na wanapaswa kuhudumiwa"

" Pesa za gharama za matibabu kutoka kwa wagonjwa zinasaidia mambo mengine ya kiutendaji,, hivyo michango ya wadau ni muhimu pia"

" Serikali kwa upande wake inajitahidi sana kuendeleza MOI kwa vifaa tiba na gharama nyingine mbalimbali,"

" Tunawashukuru sana watu wa Coral Paints kwa msaada huu"

" Hivyo, wadau kama Insignia ni muhimu katika kuisaidia serikali ," amesema Profesa Makubi.

Ameongeza kuwa wagonjwa wakihudumiwa katika majengo yanayopendeza na mazingira mazuri hupata faraja sana.

Hivyo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa wadau muhimu na kuitikia wito pale misaada yao inapohitajika.

" Wakati nilipokuwa Mkuu wa Hospitali ya Bugando Mwanza, niliwaomba msaada na majengo yale yalipendeza sana kwa sababu yao," amesema.

"Hivyo tunaomba wadau wengine wajitokeze katika kuunga mkono jitihada za Raisi Samia Sululhu Hassan za kuhakikisha wagonjwa wetu wanapata huduma nzuri.

Profesa Makubi alikabidhiwa msaada huo na Adam Kefa, mkuu wa kitengo cha Masoko wa kampuni hiyo ambaye alisema wamefanya hivyo katika kumuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya sekta ya afya hapa nchini.

" Kazi yetu kubwa ni kupendezesha majengo na kuboresha mazingira na makazi ya watu,"

"Hivyo kwa hakika rangi hizi bora zitabadili kabisa mwonekano wa MOI na kuwapa faraja wagonjwa," amesema Kefa.

Amesema katika harakati zao za kurejesha kwa jamii ( CSR), kampuni hiyo imekuwa ikitoa misaada sehemu mbalimbali ikiwemo shuleni, hospitalini na vituo vya watoto wenye uhitaji maalum.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili ( MOI) Profesa Abel Makubi ( Kulia) akipokea moja ya ndoo za msaada wa rangi zenye thamani ya milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Masoko wa Insignia Limited Adam Kefa katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...