Na mwandishi wetu Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaj Jabir Shekimweri ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kuitikia maelekezo ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupanda miti Dodoma.

Ameseyasema hayo leo Machi 15, 2024 wakati wa zoezi la upandaji wa miti 300 katika eneo la tenki kubwa la lita milioni tatu katika Mradi wa Maji wa Nzuguni.

“Hotuba kuhusu umuhimu wa kutunza wa mazingira, umuhimu wa kupanda miti zimekuwa nyingi nadhani sasa hivi tujielekeze kwenye vitendo zaidi”. Amesema Alhaj Shekimweri

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA amesema Mamlaka imekuwa ikipokea na kutekeleza maelekezo ya kupanda miti kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kufanya Dodoma kuwa ya kijani na kutunza vyanzo vya maji.

Amesema tayari miti 2000 imeshapandwa kwa mwaka 2022, na kuanzia mwaka jana Novemba hadi kufikia leo tutakuwa tumepanda miti 2000 kwa maeneo tofauti tofauti.

Miti iliyopandwa ni Chanzo cha Maji Mzakwe 250, Nzuguni tanki dogo kupitia mbio za Mwenge miti 150, Bahi 300, Kibaigwa 400, Chamwino 300 na Kongwa 300 na leo Nzuguni miti 300 ikiwa umuhimu wake ni kutunza vyanzo vya maji kuwa endelevu na stamilivu kwa mabadiliko ya tabia nchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...