Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa Kikao chake na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Katika Ukumbi wa Waziri wabFedha, Jijini Dodoma, ambapo walijadili namna Benki na Serikali zinaweza kushirikiana kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali na PBZ.

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bw. Said Mohamed Said, akizungumza wakati wa Kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), ambapo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusimamia vizuri Taasisi za Kifedha nchini na kuwawekea mazingira rafiki ya kufanya shughuli zao. Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma ilihudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali na PBZ.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bw. Said Mohamed Said, wakiagana baada ya kikao chao ambapo walijadilina namna Benki na Serikali zinaweza kushirikiana kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali na PBZ.
Na Benny Mwaipaja, Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kupanua biashara zake hapa nchini na kuitaka Benki hiyo ishushe zaidi riba ili wananchi wakiwemo watumishi wa Umma waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na Benki hiyo.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na Uongozi wa Benki hiyo Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo walijadili namna Benki na Serikali zinaweza kushirikiana kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za Benki hiyo kwa kuhakikisha kuwa wananufaika na mazingira ya ufanyaji biashara katika Sekta hiyo ya fedha.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo, Bw. Said Mohamed Said, alisema kuwa Benki yake imeendelea kukua na kupanua huduma zake upande wa Tanzania Bara, katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Dodoma na kwamba hivi karibuni inatarajia kufungua matawi mengine katika mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Tanga na Arusha.

Bw. Said alisema kuwa Benki yake imeendelea kukua na katika kipindi cha miaka mitatu sasa ilipata faida ya shilingi bilioni 75 kabla ya kulipa kodi, ina mali zisizohakishika zenye thamani ya shilingi trilioni 2 na katika kipindi hicho imetoa mikopo inayofikia zaidi ya shilingi bilioni 194.

Aliniomba Wizara ya Fedha iisaidie Benki hiyo iingizwe kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektroniki wa GePG, kwa ajili ya kukusanya malipo ya Serikali na kuangalia namna ya kupunguza baadhi ya gharama ili waendelee kutoa mikopo kwa riba nafuu kwa wateja wao kama ilivyodhamira ya Benki hiyo inayomilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...